Jifunze kuweka akiba ya Kifedha kila
mwezi na Kuilinda.
Usipoweka Akiba wakati Mungu
anakubarikia au amekubarikia ni Dhahiri pia miaka saba ijayo (Asomaye na
Afahamu)unajitengenezea mazingira ya kuuza hata ulivyo navyo vya Thamani kwa
bei ya Hasara...
Neno .1Timotheo 6:17-19.
Pigia
mstari Verse No.19
Huku mkijiwekea AKIBA, iwe msingi
mzuri kwa wakati UJAO.
Mkakati
2.
Hakikisha Akiba ya Kifedha Unayoweka
inakuwa na Utaratibu maalumu wa kimkakati katika Kiuwekezaji ili kufikia au kutimiza malengo kusudiwa KIUWEKEZAJI
Naamisha weka akiba kulingana na
Count Cost ya Project au Biashara unayotaka Kufanya, au weka akiba Kimalengo..
(Kama kwa mwaka unataka Return on Invest iwe 1,000,000, kulingana na kipato
chako basi ni dhahiri uwe na kiwango cha Kuanzia kuweka akiba kila mwezi)
Usiweke akiba isiyokuwa na Malengo
HAUTAILINDA!
(1Nyk 29:16,19)Akiba Kimalengo
Mkakati no 3.
Hakikisha unamuomba Mungu ndani ya
Moyo wako Akuweke Moyo Mkamilifu ili uwe na Hekima ya Kitumia Akiba katika
Malengo Mahususi na Sio Vinginevyo.
Daudi alimwombea Mwanae Awe na Moyo
Mkamlifu na Hekima ili Kufuata maelekezo ya Mungu pamoja na Kuijenga Nyumba
(Kama pRoject kwake au katika Ufalme wake)aliyoiwekea AKIBA.
Note:AKIBA SIO FEDHA ZA ZIADA AU
VITU VYA ZIADA IJAPOKUWA INAWEKA IKAINGIA KAYIKA HALI YA AKIBA
AKIBA NI MPANGO MKAKATI WA VITU
INAVYOPATA ILI vikufae kwa wakati Ujao
Mkakati
No.4
Akiba Inabeba maelekezo, USIWEKE
AKIBA BILA MAELEKEZO KIMAANDISHI.
DAUDI aliweka Akiba kwa ajili ya
Kujenga Nyumba ya Bwana, Lakini Akiba Hiyo ilimfanya aachilie maelekezo ya
Kimungu kwa Mwanae Suleiman.
1Nkt 22:3,5,14
Asomaye na Afahamu.
Mwisho.
Kwa uchache ulionao, unaweka ukaweka
akiba kabisa, Cha Msingi Weka akiba Kimalengo na Iwe yenye Kukupa Faida,
Kumbuka katika SHIDA Daudi aliweka akiba kwa lengo la KUJENGA NYUMBA YA BWANA
(1Nyk 22:14)
Na Muombe Mungu akufundishe ili Uone
faida na kuipata.
Isaya 48:17
Mimi ni BWANA, Mungu wako,
nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata
Utaratibu wa Kimalengo katika
uwekaji wa Akiba:
- Rule 1.
Jifunze au Jizoeshe kuweka akiba ya
Kifedha kwa Kila mafanikio yako au unachopata kwa jinsi ya Thamani ya Fedha,
Walau katika Wiki, Mara Moja na katika Mwezi Mara Nne Kithamani.kama unaweka
40000 kwa wiki, unawekeza 120000 kwa mwezi katika Ujumla wake.
Mwnzo 41:36
Kwa kile walichokipata waliweka
akiba yao kwa malengo yaliyofungwa kwa miaka 7
- Rule 2.
Jifunze kugeuza akiba unayoweka kama
"Nafaka" ili iwe "Chakula" kwa ajili ya baadae..
Akiba huchakatwa kimalengo ili
kugeuza akiba hiyoniwe yenye kufaa au thamani njema hapo baadae, Usiweke Akiba
Nje ya Malengo uliyonayo, Akiba kimalengo yanakupa Msuli wa kuchakata akiba
kuwa Chakula.
Mwanzo 41:35 pigia mstari
"Akiba ya Nafaka"
Asomaye na Afahamu
- Rule 3.
Jifunze kuweka akiba kwa jinsi ya
Wakati uliokusudiwa kimalengo,
Ifanye sehemu ya akiba yako mara
baada ya muda fulani IZAE AU IONGEZEKE kwa sababu kila akiba imebeba Nyakati
zilizokusudiwa.
1Samweli 9:23 "lete ile sehemu
nliyokupa, hiyo (alichopewa)niliyokuambia ,IWEKA AKIBA
(Sehemu ya Akiba katika Akiba kwa
wakati uliokusudiwa -1Sam 9:24)
- Rule 4.
Epuka kutumia akiba uliyoweka kabla
ya muda wake, na kinyume na malengo ndani ya akiba na nje ya muda
uliokusudiwa.
Kila akiba Kimalengo imebeba
Kusudio, muda uliokusudiwa na utekelezaji wa kimalengo.
Ukitumia kabla ya muda ni dhahiri ya
kuwa akiba yako ipo nje ya muda wa kimalengo uliokusudiwa.
Mungu Akubariki Sana