Monday, 4 December 2017

MISINGI KADHAA YA KUKUPA UFAHAMU ANGALAU UJUE NAMNA YA KUMALIZIA JAMBO ULILONALO AU WAZO LILILOKO NDANI YAKO KWA NAMNA YA KIMUNGU



Msingi wa nne
Thamini ulichonacho kwanza kwa jinsi ya Mungu ukiamini kuwa akupaye hicho ni Yeye ili ujue namna gani utakitathaminisha hicho ulicho nacho kama thamani ya kukiongezea thamani yake ili usiwe mwepesi kuishia njiani
Kwa sababu “aliye nacho atapewa zaidi(aliye ona uthamani wa hicho kidogo alicho nacho kitathaminisha hicho na kuongeza thamani) na asiye nacho , na hata hicho kidogo alicho nacho atanyang’anywa( asiye ona thamani ya alichonacho, hata akitaka kukizalisha alicho nacho itafikia sehemu atakwama tu kama sio kuishiwa kabisa) Mrk 4:25
Linganisha na hapa “Ukiwa mwaminifu kwa hicho kidogo ulicho nacho au ulicho kianzisha basi ni rahisi sana kuwa navyo vingi na kwa sababu hiyo uaminifu wako hukufanya uwe msimamizi kwa hivyo vingi utakavyo pata ,kinyume chake usipokuwa mwaminifu kwa hicho ulichonacho si rahisi kuweka matumaini ya kuapata zaidi ya hicho ulicho nacho na ifikapo wakati wa taabu  utakwama hakika na kuvunjika (Mithali25:19)
Cheki
      Mtu mwaminifu atakuwa na Baraka(guvu ya kufanya vitu na kumaliza na kukupa utajiri tele, kumbu 8:17-18) tele (mithali 28:20a)
          Thamini mbegu uliyo nayo ndani kwa itakupa thamani ya kuithaminisha kiutekelezaji ili ikupe matokeo kulingana na Thamani uliyoiweka kwenye mbegu kwa kumuhusisha Mungu, kwa sabau wazo la kukufanikisha linatoka kwa Mungu
         Kwa kuwa Mbegu yako Mungu huipa mwili(matunda) kama apendavo (1Kor 15:37-38) na apandaye si kitu wala atiaye maji ila Mungu akuzaye, Maana sisi hufanya kazi pamoja na Mungu (1Kor 3:7-9)
Msingi wa tano
   Jua aina ya watu wa kuhusiana nao wakiwa rafiki kama kweli wamebeba jambo la kujifunza kutoka kwao kulingana na jambo ulilonalo nalo ili mara nyingine ulichojifunza kikutie moyo na kukupa nguvu ya ksonga mbele pale unapokwama
      Yesu alifikia sehemu akiwa na huzuni sana na kufadhaika kutokana na ugumu wa kazi ya msalaba mbele, akawachukua akina Petro, Yakobo na Yohana wakakaa pamoja naye wampe company ya kuomba, lakini walikuwa wamelala (Mrk 14:33-38)
    Sasa cheki kama ulio nao wana uwezo wa kushikamana na wewe katika kila hali kwenye hilo jambo maana wengine watalala njiani na kukuacha mwenyewe
       Cheki kama wana “Stamina” ndani yao ya kuikabili changamoto utakayo kutana nayo na kukutia moyo ili usonge mbele
       Lakini, jifunze kutokuwa mtegemezi kwao ili kufanikisha jambo au kazi iliyoko mbele yako, si kila rafiki uliye naye ni rafiki mwenye msaada kwako, wengine ni wataabishaji(Ayubu 16:2-3)
      Lakini pia ona furaha ya Bwana kwenye hilo jambo kwa namna ya kukufanikisha, maana Furaha ya Bwana ikakuja na NGUVU YA KUMALIZA JAMBO(Nehemia 8:10)
Msingi wa sita
Jifunze kumpa Mungu nafasi yake kwa kuwa yeye aliyekupa wazo,namna ya kutekeleza ndiye atakayeikamilisha njio hiyo ya utekelezaji

Ukitaka kuwa mkamilifu katika utendaji wa jambo na lifanikiwe, kubali na fahamu kuwa kila wazo jema lililobeba mafanikio yako kiutekelezaji ni la Mungu,
Tazama hapa,
Mt 17:24-27
    Yesu alimpa Petro “Njia ya utekelezaji wa kuapata fedha uliofichwa kwenye wazo la kwenda Kuvua samaki azukaye wa Kwanza(sasa utaelewa atoaye wazo ni Mungu, nay eye ndiye mwenye kuisimamia katika utekelezaji) na akifumbua mdomo wake Petro ataona shekeli, alafu akamlipie kodi yake na Petro”
       Sasa unaweza ukaelewa kuwa “Petro asinge tii na kumpa Yesu nafasi asingepata wazo”
Na kwa sababu hiyo angekuwa bado ana deni la shekeli,
Sasa ,kama Yesu anakupa wazo ndani yako, na namna ya kulitekeleza jifunze kutii na kumpa nafasi, lakini pia Mpe asilimia 50% ya kwake kwa kila tunda litakalopatikana ndani ya huo utekelezaji wa jambo lake ili usije ukakwama njiani mara uanpotekeleza jambo hilo liwe endelevu kwenye maisha yako
Swali,
  Sasa utajuaje hili jambo likifanikiwa lazima nimpe Yesu 50% ili nisikwame hapo badaye ndani ya wazo hilo hilo kiutekelezaji?


Jibu
     Cheki mazingira ya upatikanaji wa wazo na namna ya kulitekeleza na angalia matunda yake baada ya kulifanyia kazi
     Cheki changamoto uanzokutana nazo na pima kama akili zako zinaweza zikakupa majibu ya kujua namna ya kutatua changamoto hiyo
      Cheki utafauti wa wazo na aina ya watu ulioko nao kama wana wazo linaloendana na la kwako na pima matunda unyoapata kama ni ya samaki wa kwanza(nikimaanisha linganisha mbegu yako na matokeo ya mbeguna hali ya kufanikiwa kwenye eneo lile)

Naamini hizi dondoo chache zitakupa kitu cha kukusaidia, Mungu akubariki sana

kupata misingi iliyopita Bofya hapa
Msingi wa tatu 

MISINGI KADHAA YA KUKUPA UFAHAMU ANGALAU UJUE NAMNA YA KUMALIZIA JAMBO ULILONALO AU WAZO LILILOKO NDANI YAKO KWA NAMNA YA KIMUNGU



Msingi wa tatu

    Kuwa na maarifa ya kutosha kuhusiana na hilo jambo ambalo unalianzisha kwa kuona matokeo (archievements) ili kukusukuma zaidi katika kuongeza ufahamu katika jambo hilo
“kimatokeo, utajifunza uthamani wa hilo jambo na ukubwa wake na kukupa akili yenye akili ya namna ya kulikamilisha”
Isaya 46:10 “Nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale..shauri langu litasimama, name nitatenda mapenzi yangu yote”
      Kwenye maarifa(siri ndani ya neno) kuna mwanga (Ufahamu), kuwa na wazo ni mbegu, usipojua namna ya kuipanda mbegu, wapi na udongo gani na majira gani na wakati gani na usipojua matokea ya mbegu kama chakula kwa kiwango gani ni rahisi sana kuishia njiani(Zab 119:105)
      Kwa sababu “Ufahamu mwema huleta  upendeleo” na moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa na ufahamu ni chemichemi ya UZIMA  kwake yeye aliye nao(Mithali 13:15a,15:14a,16:22a)
    Kumbuka pia ukiwa na ufahamu kwa kiwango stahiki ni lazima jambo lako lidhibitike hakika (mithali 24:3)
Tazama mfano huu
        Mpanzi (Mwenye mradi wa kimaendeleo) alikuwa na mbegu(wazo la kuzaa jambo la kumfanikisha) na mbegu hiyo akafanya kwanza uchunguzi kwa kuiweka katika makundi manne lakini kundi moja tu lilimzalia  matunda bora na mema  na kuona faida ya mbegu hiyo)kwa hiyo
Unaweza ukawa na wazo kama mbegu ndani yako na ukawa una ufahamu wa eneo moja lazima ukwame
Unaweza ukawa na mbegu lakini ukawa mvivu wa kutafuta aina tofauti tofauti ya ufahamu wa mbegu uliyo nayo kwa sababu hiyo lazima uishie njiani tuu
Unaweza ukawa na mbegu (wazo)usione umihmu wa mbegu hiyo na ukashindwa kujua aina ya udongo wa kupanda mbegu yako na kwa sababu hiyo utaishia njiani na wazo lako
Unaweza ukawa na mbegu na ukawa na ukakosa ufahamu wa mahala sahihi pa kupanda mbegu , kwa hiyo utakwama tuu njiani

Swali,
    Jee kwa nini mbegu hiyo hiyo ya aina moja iliwekwa kwenye maeneo manne tofauti na sehemu moja tu mbegu lizaa matunda? (Mt 13:3-8)
    Kuwa na ufahamu wa kutosha na chanzo zaidi ya kimoja cha maarifa kuhusu jambo lako itakusidia kuafanya “visibility study” na kukupa maarifa zaidi ya namna na wapi pa kupanda mbegu yako na kukufanikisha
     (Pilot study imejaa maarifa ya namna ya kufanikisha jambo bila kukwama, na Pilot study ipo kwa watu sahihi wa namna yako wale waliokutangulia sio kwa kuiga ila kwa kutafuta maarifa, kuiga kwingi hukwamisha watu)
kupata Misingi iliyopita bofya hapa
Msingi wa kwanza
Msingi wa pili

itaendelea msingi wa nne..
MUNGU AKUBARIKI SANA

NADHIRI

MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI NENO; Mhubiri 5:4 “ wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa” Maombi...