Msingi wa tatu
Kuwa na maarifa ya kutosha kuhusiana na hilo jambo ambalo unalianzisha
kwa kuona matokeo (archievements) ili kukusukuma zaidi katika kuongeza ufahamu
katika jambo hilo
“kimatokeo, utajifunza uthamani wa
hilo jambo na ukubwa wake na kukupa akili yenye akili ya namna ya
kulikamilisha”
Isaya 46:10 “Nitangazaye mwisho tangu
mwanzo, na tangu zamani za kale..shauri langu litasimama, name nitatenda
mapenzi yangu yote”
Kwenye maarifa(siri ndani ya neno) kuna mwanga (Ufahamu), kuwa na wazo
ni mbegu, usipojua namna ya kuipanda mbegu, wapi na udongo gani na majira gani
na wakati gani na usipojua matokea ya mbegu kama chakula kwa kiwango gani ni
rahisi sana kuishia njiani(Zab 119:105)
Kwa sababu “Ufahamu mwema huleta
upendeleo” na moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa na ufahamu ni
chemichemi ya UZIMA kwake yeye aliye
nao(Mithali 13:15a,15:14a,16:22a)
Kumbuka pia ukiwa na ufahamu kwa kiwango stahiki ni lazima jambo lako
lidhibitike hakika (mithali 24:3)
Tazama mfano huu
Mpanzi (Mwenye mradi wa kimaendeleo)
alikuwa na mbegu(wazo la kuzaa jambo la kumfanikisha) na mbegu hiyo akafanya
kwanza uchunguzi kwa kuiweka katika makundi manne lakini kundi moja tu
lilimzalia matunda bora na mema na kuona faida ya mbegu hiyo)kwa hiyo
Unaweza ukawa na wazo kama mbegu
ndani yako na ukawa una ufahamu wa eneo moja lazima ukwame
Unaweza ukawa na mbegu lakini ukawa
mvivu wa kutafuta aina tofauti tofauti ya ufahamu wa mbegu uliyo nayo kwa
sababu hiyo lazima uishie njiani tuu
Unaweza ukawa
na mbegu (wazo)usione umihmu wa mbegu hiyo na ukashindwa kujua aina ya udongo
wa kupanda mbegu yako na kwa sababu hiyo utaishia njiani na wazo lako
Unaweza ukawa na mbegu na ukawa na
ukakosa ufahamu wa mahala sahihi pa kupanda mbegu , kwa hiyo utakwama tuu
njiani
Swali,
Jee kwa nini mbegu hiyo hiyo ya
aina moja iliwekwa kwenye maeneo manne tofauti na sehemu moja tu mbegu lizaa
matunda? (Mt 13:3-8)
Kuwa na ufahamu wa kutosha na chanzo zaidi ya kimoja cha maarifa kuhusu
jambo lako itakusidia kuafanya “visibility study” na kukupa maarifa zaidi ya
namna na wapi pa kupanda mbegu yako na kukufanikisha
(Pilot study imejaa maarifa ya namna ya kufanikisha jambo bila kukwama,
na Pilot study ipo kwa watu sahihi wa namna yako wale waliokutangulia sio kwa
kuiga ila kwa kutafuta maarifa, kuiga kwingi hukwamisha watu)
kupata Misingi iliyopita bofya hapa
Msingi wa kwanza
Msingi wa pili
kupata Misingi iliyopita bofya hapa
Msingi wa kwanza
Msingi wa pili
itaendelea msingi wa nne..
MUNGU AKUBARIKI SANA