Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu
daima.
Katika Bwana nafsi
yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
Mtukuzeni Bwana
pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta Bwana
akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.
Wakamwelekea macho
wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya.
Maskini huyu aliita,
Bwana akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.
Malaika wa Bwana
hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Onjeni mwone ya kuwa
Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
Mcheni Bwana, enyi
watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
Wana-simba
hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu cho chote
kilicho chema.
Njoni, enyi wana,
mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha Bwana.
Ni nani mtu yule
apendezwaye na uzima, Apendaye siku nyingi apate kuona mema?
Uuzuie ulimi wako na
mabaya, Na midomo yako na kusema hila.
Uache mabaya
ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.
Macho ya Bwana
huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.
Uso wa Bwana ni juu
ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
Walilia, naye Bwana
akasikia, Akawaponya na taabu zao zote.
Bwana yu karibu nao
waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.
Mateso ya mwenye
haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.
Huihifadhi mifupa
yake yote, Haukuvunjika hata mmoja.
Uovu utamwua asiye
haki, Nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa.
Bwana huzikomboa
nafsi za watumishi wake, Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao