Sunday, 27 July 2014

JIFUNZE KUWA NA MOYO WA MSAMAHA ILI MUNGU AKUFANIKISHE KIKAMILIFU



Mwawezaje kutembea pamoja mkiwa hamjapatana?
Amosi.3;3
Hili ni swali ambalo  Amosi alikuwa anawambia wana wa Israel na jamaa zao.. fikra kama ndani yenu hamna upendo..na upendo hujengeka ndani ya mtu binafsi na si kwa sababu Fulani..maana upendo wa visababu haudumu.
Amos alisisitiza jambo hili ju ya upendo baina ya ndugu au mtu na mtu.swali juu yako Je mwawezaje kuishi pamoja kama huna moyo wa msamaha?Jambo la kuzingatia…fikra ..mawazo..na mtazamo….zisipoenda pamoja  hakika Baraka za MUNGU  haviwezi zikakaa kwenu..
Yakupasa muishi maisha ya upendo na roho ya msamaha ili Mung afanye makazi ndani yenu maan pasipo kuwa hivyo ni mlangon tosha wa kufunga Baraka za Mungu kwenye maisha yenu au ya mtu binafsi.Malengo ya kimaisha hayawezi kutimia kama ndani yako au yenu hamna moyo wenye upendo na msamaha maana Mungu na Baraka zake zinakaa mahali penye utulivu wa moyo na upatanisho…
Neno kutembea pamoja lina maana ya
  A)upendo halisi ndani yenu au baina yenu.
 B)kuchukuliana na kuwa na fikra patanifu.
 C)pasipo matengano yaani mioyo yenye kunai mamaja pasipo utengano.
kimtazamo neon hili lina maana ya hamwezi mkakaa pamoja na nia na mtazamo na
Jilindeni! Kama ndugu yako akikosa, mwonye. Akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe
Yesu anatutazamia kuwasamehe waamini wenzetu, wakati wanapotubu. TUnapoomba na kusema, “Utusamehe deni zetu kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu” tunamwomba Mungu atutendee kama ambavyo na sisi tumewatendea wengine. Hatutazamii Yeye atusamehe kama hatutaomba. Basi, mbona sisi tudhani kwamba anatutazamia kuwasamehe wale wasio-omba?
Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako, bali umpende jirani yako kama nafsi yako. Mimi ndimi BWANA (Walawi 19:17, 18.)
Msamaha ni njia pekee ya watu kuwa pamoja pale wanapokoseana..na hapo ndipo kuna upatanisho
Mahusiano mazuri huachilia mifumo na mitazamo mipya ya kiamafanikio katika maisha,Moyo wa mtu hunawiri palipo na mahusiano mazuri maana hapo ndipo penye tulizo la moyo..(efeso 4;31.mt 5;21) 


Neno la msingi  “Tafuteni kwa bidii kuwa na amanina watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwanaasipokuwa nao.” Waebrania 12:14. Hatuwezi kuwa na amani na watu wote kama hatuna uhusiano mzuri na Mungu. Biblia inatuonyesha mifano ya watu wengi waliokuwa na uhusiano mzuri na Mungu jinsi walivyokuwa na amani na watu wote. Tukianza na Yusufu mwana wa Yakobo, pamoja na kuuzwa utumwani na ndugu zakeambao walikuwa wakimchukia, bado aliendelea kuwa na amani nao pale walipomkuta ni kiongozi mkubwa nchini Misri (Mwanzo 37, 38, 39). Pia tunamuona mtumishi wa Mungu Stefano katikati ya maumivu ya kupigwa na mawe hata kufa bado na yeye alikuwa na amani na watu wale waliokuwa wakimpiga na kuwaombea kwa Mungu asiwahesabie dhambi ile. Hata Bwana wetu Yesu Kristo katikati ya mateso makubwa ya dhihaka na aibu, alipongongomewa msalabani na kuchomwa mkuki ubavuni bado aliendelea kuwa na amani na watu wote naye akawaombea kwa Baba. “Yesu akasema, Baba uwasamehe,kwa kuwa hawajui walitendalo...” Luka 23:34.
Ni maombi yangu kwa Mungu kwamba mimi na wewe  tujifunze na zaidi sana tuwe na uhusiano mzuri na Mungu ili tuwezekuwa na amani na watu wote pamoja na utakatifu na siku moja tumwone
Bwana Mungu mbinguni. Kama viumbe tumeumbwa tuhusiane kwa namna moja au nyingine ili
kufanya dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi.Kama wanadamu tunahusiana na watu, vitu, viumbe hai na visivyo hai pamoja na mazingira yanayotuzunguka. Basi uhusiano ni kitu cha muhimu sana kujifunza.

“Wapenzi na tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa mungu; na kila
apendaye amezaliwa na mungu naye anamjua mungu.Yeye asiyependa
hakumjua mungu, kwa maana mungu ni upendo.”
Yohana 4:7-8

Mungu akubariki sana.
  Na mwl.Fredrick J Lupenza

NADHIRI

MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI NENO; Mhubiri 5:4 “ wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa” Maombi...