SOMO: UKWELI KUHUSU PESA; SIRI MBILI ZINAZOTAWALA PESA
UTANGULIZI
Ni jambo la muhimu sana kwa kanisa la siku za mwisho kujifunza kuhusu fedha na uchumi kwa ujumla.
Ni jambo la muhimu sana kwa kanisa la siku za mwisho kujifunza kuhusu fedha na uchumi kwa ujumla.
Uamsho unaokuja wa siku za mwisho utakaopelekea KILA GOTI KUPIGWA NA KILA ULIMI KUKIRI YA KUWA YESU NI BWANA utahitaji pesa na vitendea kazi vya mabilioni na matrilioni kuipeleka injili ya Yesu, Kujenga makanisa, kuweka huduma za kijamii; NALIKUWA UCHI UKANIVIKA, NALIKUWA GEREZANI UKAJA KUNIONA, NALIKUWA MGONJWA UKAJA KUNITAZAMA, NALIKUWA NA KIU UKANINYWESHA, NALIKUWA NA NJAA UKANILISHA… Yote haya yatahitaji pesa.
![]() |
Mwalimu Dickson Kabigumila |
Gharama za kuipeleka injili kupitia mitandao, simu, redio, televisheni,
satelaiti, website nakadhalika, itahitaji pesa. Lakini pia mahitaji yetu
ya kila siku kama Wana wa Mungu yanahitaji na yatahitaji pesa
kuyaendesha [Hautanunua sukari, mafuta, ada za watoto, mahitaji ya
familia kwa kunena kwa lugha tu]; Fedha itahitajika ili kuleta JAWABU LA
MAMBO YOTE.
Hivyo basi na tuanze kwa msaada wa Roho wa Mungu kujifunza siri hizi mbili: 1.Pesa si zile SARAFU AU NOTI… Bali pesa ni THAMANI YA MWENYE NAZO anavyotazama zile sarafu na noti na KUZIPIMA NA KUZIOANISHA na HALI YA UCHUMI ILIYOPO na HALI YA UCHUMI WA UFALME WA MUNGU.
Hivyo basi na tuanze kwa msaada wa Roho wa Mungu kujifunza siri hizi mbili: 1.Pesa si zile SARAFU AU NOTI… Bali pesa ni THAMANI YA MWENYE NAZO anavyotazama zile sarafu na noti na KUZIPIMA NA KUZIOANISHA na HALI YA UCHUMI ILIYOPO na HALI YA UCHUMI WA UFALME WA MUNGU.
*Rula inapima urefu; Ila rula si urefu, ndio maana hata ukiondoa rula, kama ni sentimeta 2 zitaendelea kuwa sentimeta 2, haziathiriwi na uwepo au kutokuwepo kwa rula.
*Mzani unapima uzito; Ila mzani si uzito, ndio maana kama umepima kitu kina kilogram 5 juu ya mzani hata ukiondoa kwenye mzani pia uzito wake utabaki kuwa kilogram 5.
“Ndivyo ilivyo pesa; kama THAMANI YA MWENYE NOTI AU SARAFU ni kubwa akiwa na NOTI AU SARAFU itabaki kuwa kubwa hata hizo NOTI NA SARAFU zikiondoka. Na ndivyo ilivyo kinyume chake”
NAKUFUNDISHA UCHUMI KWA UFUNUO NA SI VITABU AU KANUNI ZA DUNIA HII. 2. Pesa haikai mahali ambako HAINA CHA KUISHIKA.
Watu wa dunia hii wanaotawala uchumi na pesa wanaelewa wazi kwamba ili pesa ibaki lazima iwe na cha kuishika na kinaitwa “KI/VITEGA UCHUMI” na kadri unavyokuwa navyo vingi ndivyo unavyokuwa na UWANJA MPANA wa kutawala MZUNGUKO WA PESA na KUONGEZA PESA toka mikononi mwa WASIO NA VITEGA UCHUMI… Kwa kifupi, KITEGA UCHUMI ni bidhaa au huduma inayotimiza mahitaji ya watu KWA MABADILISHANO NA PESA toka kwa wahitaji bidhaa au huduma.
HII NDIYO NJIA YA KIBINADAMU ILIYOWEKWA NA MUNGU KUZALISHA FEDHA [Rejea mfano wa talanta].
Kwenye Ufalme wa Mungu:
Mbali ya VITEGA UCHUMI kinachoweza kuishika PESA IKAE ni MUNGU NA KANUNI ZA MZUNGUKO WA PESA alizoweka ambazo zinaitwa UTOAJI.
Mbali ya VITEGA UCHUMI kinachoweza kuishika PESA IKAE ni MUNGU NA KANUNI ZA MZUNGUKO WA PESA alizoweka ambazo zinaitwa UTOAJI.
Mungu kama Mungu binafsi YEYE MWENYEWE ni SUMAKU inayovuta na kunasa uchumi na fedha.
Ukilisoma Neno la Mungu utagundua kwamba, “FEDHA NI MALI YAKE; DHAHABU
NI MALI YAKE; VYOTE VIIJAZAVYO NCHI NI MALI YAKE; DUNIA NA WOTE WAKAAO
NDANI YAKE”
Hii ni siri ya ajabu kwa mtu anayetaka kuwa na uchumi mkubwa. KITEGA
UCHUMI kikubwa na cha kwanza unachokihitaji KUVUTA PESA NA UCHUMI MZURI
ni MUNGU ALIYE HAI.
“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya UTAJIRI WAKE katika utukufu katika Kristo Yesu” (Wafilipi 4:19).
“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya UTAJIRI WAKE katika utukufu katika Kristo Yesu” (Wafilipi 4:19).
“Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, Yaani, Wamchao [BWANA] HAWAHITAJI
KITU [kwa maana wana zaidi ya wanavyohitaji toka mikononi kwa BWANA]”
(Zaburi 34:9).
“Wana-simba hutindikiwa huona njaa; Bali WAMTAFUTAO BWANA HAWAHITAJI
KITU CHOCHOTE KILICHO CHEMA [wana kila kitu na kuzidi]” (Zaburi 34:10).
“…Usije ukamsahau BWANA, Mungu wako AKUPAYE NGUVU [za kiroho, kiakili,
kimawazo, kiubunifu, kiuzalishaji, kiafya] ZA KUUPATA UTAJIRI”
(Kumbukumbu 8:18).
“UTAJIRI NA HESHIMA ZIKO KWANGU [MIMI MUNGU], Naam UTAJIRI UDUMUO, na haki pia” (Mithali 8:18).
“[Mimi Mungu] natembea katika NJIA YA HAKI, katikati ya MAPITO YA
HUKUMU. Niwarithishe MALI wale WANIPENDAO, TENA NIPATE KUZIJAZA HAZINA
ZAO” (Mithali 8:20-21).
Njia ya pili kwenye Ufalme wa Mungu ya kutunza pesa ni kupitia SADAKA/ UTOAJI:
a)Fungu la kumi (Malaki 3:8-12)
a)Fungu la kumi (Malaki 3:8-12)
-Kufungua mbingu ziwe wazi upande wa mtoaji
-Kufanya mbingu ziachilie baraka zaidi ya uhitaji na kiwango cha kupokea cha mtoaji
-Kuzuia chanzo cha mapato kisishambuliwe na adui/ alaye
-Kumfanya mtoaji wa fungu la kumi atambulike na kutofautishwa na watu
wengine wa kawaida [Na mataifa yote watakuita heri/ aliyebarikiwa].
b)Kutoa kwa masikini/ kumsaidia asiye na uwezo/ aliye na uhitaji (Mithali 19:17, Zaburi 41:1-3, Mithali 21:13).
-Kumsaidia masikini kwa huruma [compassion] ni mkopo kwa Mungu
anaolazimika kuulipa; Mungu anachukia madeni, hawezi kukubali kuwa mdeni
kwa mtoaji, hivyo lazima alipe na RIBA juu
-Kumsaidia masikini NI UWEKEZAJI KWA AJILI YA SIKU YA TABU [Nyakati
mbaya] na itaufanya mkono wa Mungu ukusaidie wakati wa Magumu na taabu.
-Kumsaidia Mhitaji na masikini ni MBEGU itakayotoa matunda WAKATI WA UHITAJI WAKO; Utaita na Mungu atakusikia na kukusaidia
-Kuwasaidia masikini na wahitaji ni njia ya KUWEKA WIGO WA ULINZI wa Mungu kwenye maisha yako, familia, watoto na mali yako.
Ayubu alikuwa BABA KWA YATIMA, MME KWA WAJANE NA JIBU LA WAHITAJI na ikapelekea Mungu KUMJENGEA WIGO dhidi ya kila hila na shambulizi la adui zake. c)Kutoa kwenye Injili, Shughuli za Kuujenga Ufalme wa Mungu / Mambo yanayomhusisha Yesu (Marko 10:28-30).
Ayubu alikuwa BABA KWA YATIMA, MME KWA WAJANE NA JIBU LA WAHITAJI na ikapelekea Mungu KUMJENGEA WIGO dhidi ya kila hila na shambulizi la adui zake. c)Kutoa kwenye Injili, Shughuli za Kuujenga Ufalme wa Mungu / Mambo yanayomhusisha Yesu (Marko 10:28-30).
-Mtoaji ana uhakika wa kupata mara mia hapa duniani [a hundredfold]
kwenye kila alichotoa- Inawezekana asipate kwa mkupuo au kwa nmna
alivyotegemea kupokea lakini hakika atapata maramia ya kile alichowekeza
kwenye injili au Ufalme wa Mungu.
-Ana uhakika wa kupata chochote “alichokisadaka” kwa ajili ya Yesu na
injili; Yawe mahusiano [Baba, mama, ndugu wake na waume], Mali [Nyumba,
mashamba] nakadhalika mara mia hapahapa duniani.
LAKINI JIANDAE
Utaoji huu una malipo ya juu sana, yanayozidi kawaida hivyo watu wanaokuzunguka hawataelewa “Unafanyafanyaje” kuzungusha uchumi wako, hivyo UTAPATA UDHIA [Kusemwa, kusingiziwa, lawama na kila lisilopendeza] kwa maana kuipeleka injili na Yesu ni KUTANGAZA VITA YA MOJA KWA MOJA NA SHETANI. Ni kuipeleka nuru na kuling’oa giza. Ni kuuondoa Ufalme wa shetani na kuujenga Ufalme wa Yesu Kristo.
KUZIMU YOTE ITAJARIBU KUKUZUIA usiendelee kuleta madhara; UKIONA HIVI KAZA UZI, ONGEZA UTOAJI WAKO… Hii ni sehemu ya utoaji huu wa baraka sana!! Siri hizi mbili zitafakari ni za muhimu sana kwako Mkristo unayetaka kuwa na mahusiano mazuri na Mungu lakini pia kuwa na uchumi mzuri.
Wako Katika Kristo Yesu,
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mawasiliano:
Simu: 0655 466 675 [Kupiga, Whatsapp na meseji] 0753 466 675 [meseji tu] Email: dicoka@rocketmail.com
Website ya mafundisho zaidi: www.yesunibwana.org