Tuesday, 28 November 2017

NEEMA NA BIDII HUENDA PAMOJA

 Bidii, Neema, Katika Passion ya kufanya jambo ndani yako huwa ina uwezo wa kuleta matokeo ambayo yataigusa Dunia yako,

Watu wengi huwa tunajikuta na Passion(shauku) ila tunakosa vitu vya kutusaidia kuona matokeo ya shauku tukiyo nayo,
           Neema na Bidii mara nyingi huenda pamoja, ukiwa na Neema (I encounter as favor to you) ukakosa Bidii utaishia kuishi chini ya kiwango kuliko Neema iliyo maishani mwako..
Kama vile Neema unatofautiana kati yetu, hali kadhalika Bidii pia hutofautiana,
          Tofauti yetu Katika kupata Matokeo (objective achievements) ya kile tulichokusudia (Focused Purpose with Detailed) mara nyingi ipo kwenye 

1.Namna tutavyoelewa kuhusu Neema iliyo juu yetu (Utumiaji wa Neema kutufanikisha)
~kustahilishwa, kupewa usichostahili lakini ukapewa tuu, mkebe wa kukusaidia kukabiliana na aina ya mazingira yoyote utakayoishi. 

2.Bidii katika Kile ambacho Mungu amekuwekea ndani yako ili kikusaidie kukabili mazingira na kuishi bila kumwasi Mungu,
"Nilikuwa nasoma Cv ya Bishop Thomas Dexter Jakes (T.D Jakes) wakati anaanza huduma akiwa bado kijana walimwita "Kijana wa Biblia" hadi ikafikia wakati akaanza kanisa likiwa na watu 10 tu" hiyo ilikuwa Mwaka 1979, sasa cheki hakuishia hapo tuu, akaweka Bidii ili kile alichokianzisha kifikie malengo katika Bwana,
Alijua Iko Neema ya kumsaidia katika Eneo hilo la kuwa Mch. (Kuchunga kondoo wa Bwana), akaamua kwenda kufanya kazi kwenye mitaro ya maji apate fedha za kumsaidia kuendesha kanisa, na kanisa lake la Kwanza liliitwa " The Greater Emmanuel Temple of faith" ( Montgomery, West Virginia.)
    Neema na Bidii huenda pamoja, ukiwa na neema ukakosa Bidii utaishiwa kuwa wa Kawaida tuu,
Hata kwenye eneo lolote lile la maisha, Usipoweka bidii katika Kile unachokifanya utabaki pale pale miaka nenda rudi
Sasa cheki, TD Jakes ndani ya miaka kumi tangu aanzishe kanisa lake alikuwa na waumini 1000.(NEEMA +BIDII)
        Licha ya kuwa alikuwa anasoma Bible na kufundisha lakini aliweka bidii kwa kile alichonacho ili kisibaki tuu kwenye kusoma na kufundisha ila AKILEE KWA WATU ALIYOWAFUNDISHA NA KUONA WANASONGA MBELE NA KUONGEZEKA KWA KILE ALICHO WEZA KUKIWEKEZA KWAO
suala si tuu unaitwa jina fulani, suala tunataka kuona matokeo ya ulichonacho ikiwa ni Imani katika Matendo, 

         Imani - Uhakika wa kukifanya kile ukichokitumainia ndani kiwe dhahiri na sio kubaki tuu kama Nadharia
        Imani - Hufanya vile visivyo onekana vionekane na vikionekana vikue, kama kuna Imani hata imani, basi ni dhahiri kuna kuvifanya vile vinavyonekana vikue zaidi na zaidi, (Faith in working by Multi-increase Manifestation)

      Sasa Tuje kwenye Bidii,

        Ukisoma Yakobo 5:17 kuna vitu kadhaa kuhusu bidii iliyokuwa ndani ya Eliya.. Licha ya kuwa na Neema (inayomtofautisha yeye na wengine, japo ni Binadamu) lakini vipo vitu kadhaa ndani,
Mstari "Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita"
Ukisoma, utaona Neno linasema kuwa alikuwa  Mwanadamu mwenye tabia moja kama sisi
     Swali la kujiuliza kwani wanadamu wote wana tabia Moja???

Ukienda ndani zaidi kuhusu tabia ukiungaisha na bidii utagundua Biblia inazungumzia kuhusu Vitu vilivyo ndani ya nafsi maana kwenye nafsi kuna viti kadhaa ambavyo wote tunavyo, -Tofauti ipo kwenye namna tunavyo react kwa jinsi ya nje

Kwa hiyo kwenye nafsi in nature kuna

hisia, maamuzi, mawazo,( fikra au akili)

Na hivyo vyote vina mchango sana Kwenye eneo lako la Neema, aidha kukujenga au kukubomoa,
Oky, kwa hiyo.. Tofauti yetu na Eliya ipo kwa jinsi ya nje kuvitumia vile ambavyo viko ndani yake na sisi tunavyo!!
Ndo utakutana na Neno Bidii
Ngoja nikuelezee hapa,

Bidii, 

1.Inahusisha kufanya kitu kwa umakini mkubwa na kwa maelekezo sahihi ya kufanya hicho kitu au wazo linatika ndani,
Sasa cheki ndani ya nafsi kuna mawazo
Doing things in CAREFUL WITH DETAILE WAY
 
    BIDII INA VITU HIVI
CAREFULL +DETAILS (STRATEGIES)
Kwa hiyo Eliya aliomba akiwa na maelekezo maalumu naya kutosha, hakufanya Blaa blaaa

    2.Inahusiha shauku ya kutaka kuona una fikia malengo,
Sasa cheki, Shauku huanzia ndani, ndani ya mtu wa ndani, yaani nafsi,
Kwa hiyo  Enthusiasm in pursuing of an bojectives ina husisha Neno Bidii,

In nutshel Bidii pia ina vitu hivi (Shauku au hamu(enthusiasm) pamoja na Malengo maalumu kwa kipindi fulani (Objective) 

     Kwa hiyo Eliya naye aliomba, lakini alitaka kuona kile anachoomba kinatokea au kinafanikiwa kwa muda uliokusudiwa (muda unaonekana kipindi mvua haikunya-kwa jinsi ya matokeo ya alichoomba)
    3.Inahusika pia na  Seriousness with Purpose (Extremely Passionate, Fervently, very strong feelings kutoka ndani yako)
"Intensity of Spirit" hali ya kutaka jambo litokee bila kukata tamaa, mtu wa ndani kuhakikisha kile kilichokusudiwa kutoka ndani kinafikiwa, au kinafanikiwa hata kama mazingira hayakuruhusu

: Oky,
Twende taratibu, Nliposoma habar ya TD Jakes ndo ikanipa sana kutafakar kuhusu NEEMA +BIDII,
Nikagundua, licha ya kuwa mazingira yalikuwa changamoto kwake kufanya kile alichokuwa nacho ndani, lakini shauku yake ya ndani haikukwamishwa na mazingira kwa kuwa alijua kuwekeza *BIDII YAKE IPASAVYO
Alitengeneza mazingira kwa bidii yake kufika hapa alipo leo kwa utukufu wa Bwana
Hakuishia kuwa na watu kumi, ila aliweka malengo yake kwa bidii ili kufikia waumini 1000 baada ya miaka kumi!!
Alijituma kwa bidii kuona kile alichonacho ndani hakikwami hata kama mazingira hayakupa nafasi,
Nligindua pia Bidii sio Bidii kama *Haipimwi kwa muda na kwa uthubutu*
Ukisoma Maandika utagundua pia,
Bidii
  1. Ni ufunguo unavuta hali ya kutawala ndani yako kuwa mubashara kwenye eneo uliloko kwa kile unachokifanya.. Kwa kuwa bidii huamua kiwango cha shauku ukiyonayo ndani kuonekana,Mkono wa mwenye bidii utatawala Mithali 12:24a
Mkono (kile unachokifanya) hukufanya utawale kwa matunda ya kile ukifanyacho
Mwenye bidii hufadhiliwa au huelekea God's favor..
"He who diligently seeks good seeks [God's] favor," Mithali 11:27
2.   Bidii ni moja ya ufunguo wa kufikia utajiri - matunda ya kile unacho jibidisha nacho..
Kiwango chako cha bidii katika kazi au jambo au mawazo uliyonayo ndani kina amua kiwango cha matunda (product/fruits) utakayopata,
"Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.(Mithali 10:4b)
"Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.''
Mithali 13:4
Kuna Neno Nafsi,Rejea Neno Eliya alikuwa Mwanadamu mwenye tabia kama moja na sisi!!!
(Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa)
Tofauti ipo kwenye kutumia vile tukiyo Neemeshwa ili kutusaidia katika mawazo Yetu, Tunafikiri tofauti japo wote tuna Fikra
Kwa sababu hiyo Tuna jibidisha tofauti tofauti kulingana na vile tunavyo fikiri kulingana na mazingira tunayokutana nayo
"but the appetite of the diligent is abundantly supplied"
3.  Njia mojawapo pia ya kufanikiwa kwenye eneo lolote, ni kuongeza bidii (kutafuta maarifa, ubunifu, ujuzi nk) kwa kile unachokifanya au utakachokifanya,
Bishop TD Jakes ni mtu pia mwenye ujuzi kwenye mambo ya Filamu (Filmmaker), wakati anaanza, hakuishia tuu kutengeneza filamu na kuhubir ila pia kwenye uandishi wa vitabu kadhaa (30 copies mpka sasa, +) na hata kwenye studio pia!!
Neno linasema
"Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu;Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji., Mithali 21:5
In Amp. Bible
"The thoughts of the [steadily] diligent tend only to plenteousness, but everyone who is impatient and hasty hastens only to want."
"The Only Thing in my life is yo Serve you God, Living One, Jesus Chris is my Brand" John 4:34

MUNGU AKUBARIKI SANA
LUPENZA B.
SIMU +255(0)752048979- WhatApps

NADHIRI

MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI NENO; Mhubiri 5:4 “ wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa” Maombi...