Wednesday, 15 January 2020

NADHIRI




MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI
NENO;
Mhubiri 5:4 “wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa”
Maombi ya nadhiri ni maombi afanyayo mtu kwa hiari ya moyo wake juu ya jambo Fulani na unaachilia ahadi ndani ya moyo wako ambayo itamsukuma Mungu kujibu maombi yako sawasawa na muda ambao Mungu anatimiza ahadi yako.au
Ni maombi afanyayo mtu kwa hiari yake mwenyewe na Mungu anayemtumkia  kiasi cha majibu yake yamefichwa katika ahadi  ya hiari kati yake na MUNGU ambayo ndio patano lake na MUNGU. Akitafuta sana mwongozo wa Mungu, Yeftha anaweka nadhiri hii kwa Mungu: “Hakika ukiwatia wana wa Amoni mkononi mwangu, itatukia pia kwamba yule atakayetoka nje, atakayetoka nje ya milango ya nyumba yangu kuja kunipokea nitakaporudi kwa amani kutoka kwa wana wa Amoni, lazima atakuwa wa MUNGU, nami nitamtoa huyo kuwa toleo la kuteketezwa.” Waamuzi 11:30-33.
Roho ya Mungu ilikuwa ikitenda juu ya Yeftha alipoweka nadhiri hiyo, na pia MUNGU alibariki jitihada zake. Maandiko yanamsifu Yeftha kwa sababu ya imani yake na kwa yale aliyofanya kuhusiana na kusudi la Mungu. (1 Samweli 12:11; Waebrania 11:32-34)Kwa hiyo, hangefikiria hata kidogo kumtoa mwanadamu awe dhabihu. Kufanya hivyo ni uuaji. Hivyo basi, Yeftha alikuwa akifikiria nini alipoweka nadhiri ya kumtoa mtu kwa MUNGU?NADHIRI ZAKO MBELE ZA MUNGU ZISIZIDI UWEZO WAKO KIIMANI ILI KUTIMIZA
Ni wazi kwamba Yeftha alimaanisha kuwa angemtoa yule ambaye angekuja kumpokea ili amtumikie Mungu kikamili.
Hiyo ni nadhiri ambayo Yeftha aliweka kwa MUNGU..na Mungu akafanikisha..Angalia habari za Yakobo  kaweka nadhiri na ikamsukuma Mungu kujibu (Mwanzo 28;20-22)
USIWEKE NADHIRI MBELE ZA MUNGU KAMA ROHO WA MUNGU HAJAKUSHUHUDIA NDANI YAKO MATOKEO YAKE UTAKUWA NA DENI MBELE ZA MADHABAHU YA MUNGU.
VIPENGELE VYA NADHIRI MBELE ZA MUNGU
A)uwe na hoja yenye nguvu mbele za MUngu  au neon lenye nguvu isaya 41:21
B)uwe na sadaka ya hiari maana sadaka yako ni patano timilifu mbele za MUNGU.Mwanzo 28;20,1Samw.1;10-12
c)uwe na muda  muafaka wa kutoa nadhiri yako iliyobeba maombi yako
d)ukiweka nadhiri yako hakikisha unaitoa na usiweke nadhiri kama ndani yako huna uhakika wa kuitimiza maana ni suala lenye gharama kwako.Kumb.23;21-23,Zab 50.14
e)Usitoe nadhri yako mahali ambapo Mungu hajapatana nawe…kama umwemwaidi Mungu kumtolea eneo Fulani usitoe kinyume na patano lako na Mungu kwa itabaki kuwa deni mbele ya madhabahu ya MUNGU.Mwanzo 31:13,17,hesabu 30;3-16.
kumbuka yapo madhara ya kutotimiza nadhiri yako kwa MUNGU moja wapo ni
Anania na safira waliweka nadhiri yao ya kuuza kiwanja na kukabidhi fedha ila baadaye waliona tamaa na kutoweza kutimiza nadhiri yao, matokeo yake ni kifo.Unaishi katika mashaka na wasiwasi muda wote kwani nadhiri yako hujaitoa kwa Mungu.Matendo ya mitume 5:1-11..Maendeleo ya kiimani na kiuchumi yanadumaa kutokana na kutotimiza nadhiri yako.

Mungu akubariki sana
 Na mwl.Fredrick J Lupenza

Kuhusu Akiba .(Kiuchumi)

Mkakati no 1.(Kiuchumi) 
Jifunze kuweka akiba ya Kifedha kila mwezi  na Kuilinda.
Usipoweka Akiba wakati Mungu anakubarikia au amekubarikia ni Dhahiri pia miaka saba ijayo  (Asomaye na Afahamu)unajitengenezea mazingira ya kuuza hata ulivyo navyo vya Thamani kwa bei ya Hasara...
Neno .1Timotheo 6:17-19.
Pigia mstari Verse No.19
Huku mkijiwekea AKIBA, iwe msingi mzuri kwa wakati UJAO.

Mkakati 2. 
Hakikisha Akiba ya Kifedha Unayoweka inakuwa na Utaratibu maalumu wa kimkakati katika Kiuwekezaji ili kufikia au kutimiza malengo kusudiwa KIUWEKEZAJI
Naamisha weka akiba kulingana na Count Cost ya Project au Biashara unayotaka Kufanya, au weka akiba Kimalengo.. (Kama kwa mwaka unataka Return on Invest iwe 1,000,000, kulingana na kipato chako  basi ni dhahiri uwe na kiwango cha Kuanzia kuweka akiba kila mwezi)
Usiweke akiba isiyokuwa na Malengo HAUTAILINDA!
(1Nyk 29:16,19)Akiba Kimalengo

Mkakati no 3.
Hakikisha unamuomba Mungu ndani ya Moyo wako Akuweke Moyo Mkamilifu ili uwe na Hekima ya Kitumia Akiba katika Malengo Mahususi na Sio Vinginevyo.
Daudi alimwombea Mwanae Awe na Moyo Mkamlifu na Hekima ili Kufuata maelekezo ya Mungu pamoja na Kuijenga Nyumba (Kama pRoject kwake au katika Ufalme wake)aliyoiwekea AKIBA.
Note:AKIBA SIO FEDHA ZA ZIADA AU VITU VYA ZIADA IJAPOKUWA INAWEKA IKAINGIA KAYIKA HALI YA AKIBA
AKIBA NI MPANGO MKAKATI WA VITU INAVYOPATA ILI vikufae kwa wakati Ujao
  
Mkakati No.4
Akiba Inabeba maelekezo, USIWEKE AKIBA BILA MAELEKEZO KIMAANDISHI.
DAUDI aliweka Akiba kwa ajili ya Kujenga Nyumba ya Bwana, Lakini Akiba Hiyo ilimfanya aachilie maelekezo ya Kimungu kwa Mwanae Suleiman.
1Nkt 22:3,5,14
Asomaye na Afahamu.
Mwisho.
Kwa uchache ulionao, unaweka ukaweka akiba kabisa, Cha Msingi Weka akiba Kimalengo na Iwe yenye Kukupa Faida, Kumbuka katika SHIDA Daudi aliweka akiba kwa lengo la KUJENGA NYUMBA YA BWANA (1Nyk 22:14)
Na Muombe Mungu akufundishe ili Uone faida na kuipata.
Isaya 48:17
Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata

Utaratibu wa Kimalengo katika uwekaji wa Akiba:
  • Rule 1.
Jifunze au Jizoeshe kuweka akiba ya Kifedha kwa Kila mafanikio yako au unachopata kwa jinsi ya Thamani ya Fedha, Walau katika Wiki, Mara Moja na katika Mwezi Mara Nne Kithamani.kama unaweka 40000 kwa wiki, unawekeza 120000 kwa mwezi katika Ujumla wake.
Mwnzo 41:36
Kwa kile walichokipata waliweka akiba yao kwa malengo yaliyofungwa kwa miaka 7
  • Rule 2.
Jifunze kugeuza akiba unayoweka kama "Nafaka" ili iwe "Chakula" kwa ajili ya baadae..
Akiba huchakatwa kimalengo ili kugeuza akiba hiyoniwe yenye kufaa au thamani njema hapo baadae, Usiweke Akiba Nje ya Malengo uliyonayo, Akiba kimalengo yanakupa Msuli wa kuchakata akiba kuwa Chakula.
Mwanzo 41:35 pigia mstari "Akiba ya Nafaka"
Asomaye na Afahamu
  • Rule 3.
Jifunze kuweka akiba kwa jinsi ya Wakati uliokusudiwa kimalengo,
Ifanye sehemu ya akiba yako mara baada ya muda fulani IZAE AU IONGEZEKE kwa sababu kila akiba imebeba Nyakati zilizokusudiwa.
1Samweli 9:23 "lete ile sehemu nliyokupa, hiyo (alichopewa)niliyokuambia ,IWEKA AKIBA
(Sehemu ya Akiba katika Akiba kwa wakati uliokusudiwa -1Sam 9:24)
  • Rule 4.
Epuka kutumia akiba uliyoweka kabla ya muda wake, na kinyume na malengo ndani ya akiba na nje ya muda uliokusudiwa. 
Kila akiba Kimalengo imebeba Kusudio, muda uliokusudiwa na utekelezaji wa kimalengo.
Ukitumia kabla ya muda ni dhahiri ya kuwa akiba yako ipo nje ya muda wa kimalengo uliokusudiwa.
 Mungu Akubariki Sana

NADHIRI

MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI NENO; Mhubiri 5:4 “ wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa” Maombi...