Sunday, 5 November 2017

SOMO: KWA NINI WAKRISTO WENGI NI MASKINI?


SOMO: KWA NINI WAKRISTO WENGI NI MASKINI? By Mwalimu Dickson Kabigumila.

1). Wengi wanaishi maisha YA KUCHEZEA NA KUTOTHAMINI VICHACHE MUNGU ALIVYOPITISHA MAISHANI MWAO.
“Yesu alipofanya muujiza wa kulisha wanaume 5000; Chakula kilichobaki alikikusanya na ALISISITIZA KISIPOTEE HATA KIPANDE KIMOJA CHA MKATE” (Yohana 6:8-12). -Mtu yeyote ASIYETHAMINI VIDOGO MUNGU ALIVYOPITISHA MIKONONI MWAKE NA KUVIHIFADHI KWA UMAKINI NA ADABU hawezi kamwe kuwa tajiri; Atakuwa masikini milele! Je, Wewe unavitunza vitu vidogo ambavyo Mungu anavipitisha mikononi mwako au unatupa ovyo? Hauwezi kuwa na hekima ya uchumi na maisha kuliko Yesu; YEYE HAKURUHUSU HATA KIPANDE KIPOTEE! Badili hiyo tabia yako ya UFUJAJI NA UHARIBIFU KAMA UNATAKA KUTOKA KWENYE UMASIKINI. “Ni matone madogo madogo ya maji yanayotengeneza bahari kubwa ya maji unayoiona”
2). Wengi wanaishi BILA MIPANGO, WANAISHI MAISHA YA BORA LIENDE.
Je, Umewahi kumwona mjenzi yeyote aliyejenga nyumba bila ramani? Je, umewahi kumuona mjenzi yeyote aliyejenga bila kupima? Kwanini iweko RAMANI? Kwanini viweko VIPIMO MAALUMU? Jibu ni rahisi, UKITAKA KUJENGA MAISHA YAKO YA UCHUMI NA FEDHA, HAUNA TOFAUTI NA MJENZI WA NYUMBA.
Hii ndiyo sababu ukitaka mkopo benki au taasisi nyingine ya fedha watakuuliza kuhusu WAZO LA BIASHARA [business proposal and idea] ambayo wataalamu hao wa fedha wataitumia kupima UWEZO WAKO NA MIPANGILIO YAKO YA KIFEDHA inayokustahilisha kupata fedha au la! Yesu alisema, “MTU AKITAKA KUJENGA NYUMBA, HALAFU ASIHESABU KWANZA GHARAMA SAWASAWA, AKIKWAMA KUIMALIZA WATU WATAMCHEKA NA KUMDHIHAKI NA ATAPATA AIBU YA MWAKA” (Luka 14:28).
Mungu wetu ni Mungu wa Mipango; Ilipoingia dhambi kule bustanini, hapohapo alitangaza MPANGO WA WOKOVU KUPITIA UZAO WA MWANAMKE. Usipokuwa na mipango yoyote ya maana na ya kueleweka maishani, tayari umekwama na haikosi utakuwa na umasikini wa kukutosha! “UKISHINDWA KUPANGA, UMEPANGA KUSHINDWA” “Haijalishi unapata hela kiasi gani au pesa kiasi gani inapita mikononi mwako; Kama haujaipangilia na kuielekeza pa kwenda, itapotea hivyohivyo” WEKA MIPANGO YA MAISHA YAKO; HAKUNA WA KUKUPANGIA.
3). Kujaribu KUISHI MAISHA YALIYOKUZIDI.
Watu wengi wanaishi maisha ya kutaka kujionesha, kutaka kuwakoga watu au kutaka kuonesha wengine kwamba NAO WAMO. Tajiri ni yule mtu ambaye amefanikiwa KUISHI AWEZAVYO NA SI WATU WATAKAVYO. Tajiri ni yule anayeishi kwenye ndoto zake na maono yake bila kujali watu wanamuelewa au hawamuelewi. Tajiri ni mtu anayeishi maisha yake halisi kwa wakati uliopo. Biblia inasema, “UTAUWA NA KURIDHIKA NI DAWA BORA….” (1Timotheo 6:6). Mtu atakayekuwa na MOYO WA KURIDHIKA NA KUTOJARIBU Kuishi maisha yasiyokuwa yake, Maisha yaliyomzidi; Mtu asiyeishi maisha ya kujikweza, huyu ndiye atakayekuwa na MAISHA MAZURI YA UCHUMI. “Ridhika na hali yako uliyonayo sasa na usijaribu kukopa au kuomba ili uishi maisha ya juu”
4). Kutokupenda KUFANYA KAZI NA UVIVU.
Unajua kuna watu wanatoa sana ZAKA NA DHABIHU lakini hawapati matokeo kwenye maisha yao; HAWANA “CHANEL/ MKONDO” ambao Mungu atautumia KUWAPATIA BARAKA ZAO. Hawana GHALA ambayo MUNGU ATAIMIMINIA BARAKA MPAKA KUSIWEKO NAFASI (Malaki 3:10). Hawana KAPU LA UNGA ambalo MUNGU ATALIBARIKI ILI LISIISHIWE (Kumbukumbu 28). Hawana MZABIBU ambao MUNGU ATAULINDA USIPUKUTISHE KABLA YA WAKATI WAKE (Malaki 3:11), Hawana HAZINA [VITEGA UCHUMI] amabazo MUNGU ATAZIJAZA (Mithali 3:9-10). Kanuni ya Biblia inasema, “USIPOFANYA KAZI NA USILE” (2Thesalonike 3:10-11). Hata mimi mtumishi wa Mungu nafanya kazi yangu kwa bidii na Mungu ananitunza na kukutana na maisha yangu hukuhuku madhabahuni, USIPOKUWA NA SHUGHULI YA KUFANYA, UNAMBANA MUNGU ASIPATE MKONDO WA KUPITISHIA BARAKA ZAKO baada ya kutoa ZAKA NA DHABIHU ZAKO… Mungu anataka kubariki CHANZO CHA MAPATO YAKO; Hivyo usipofanya kazi, Usipojishughulisha, UNAZUIA upako wa wa Mungu kukupa utajiri! “FANYA KAZI NA FUNGUA VYANZO VYA UCHUMI AMBAVYO MUNGU ATAVITUMIA KUPITISHIA BARAKA ZAKO; UWE NA HAZINA ATAKAYOIJAZA BWANA; UWE NA KAPU LA UNGA ATAKALOLIBARIKI MUNGU” Kufanya kazi ni lazima, Iwe ya kujiajiria au kuajiriwa!
5). MTAZAMO NA IMANI POTOFU KUHUSU UTAJIRI, MALI NA PESA.
Makanisa mengi yanapinga habari ya utajiri na pesa. Wengi utawasikia wakisema, “Hizi injili za utajiri si nzuri zinapotosha watu” Lakini Yesu alisema, “NIMEKUJA ILI WAWE NA MAISHA KISHA WAWE NAYO KWA KIWANGO CHA JUU SANA” (Yohana 10:10 Biblia za Kiingereza). Yesu alipoanza kuhubiri Injili alisema, “NIMEKUJA KUWAHUBIRIA MASIKINI HABARI NJEMA” (Luka 4:18-19), HABARI NJEMA KWA MASIKINI NI KUMTOA KWENYE HALI YAKE MBAYA ALIYONAYO KIROHO KWANZA HALAFU KIUCHUMI. Hii ndiyo Injili halisi aliyoileta Yesu, Haikatazi watu kuwa na UCHUMI MZURI NA MKUBWA. Ukisoma Kitabu cha Yakobo, Biblia inatwambia, “NDUGU YAKO AKIWA UCHI UMVIKE NA USISEME ENENDA KWA AMANI UKAOTE MOTO NA MUNGU ATAKUSAIDIA” Lakini hii ndiyo INJILI tunayohubiri makanisani.
HATUNA MAJIBU YA KIUCHUMI NA MAHITAJI YA WATU WASIOJIWEZA; HII SI SAHIHI. Yesu na wanafunzi wake WALIKUWA NA HUDUMA YA KUWASAIDIA WASIOJIWEZA. Mitume wa Yesu WALIKUWA NA HUDUMA YA KUWASAIDIA NA KUWATUNZA WASIOJIWEZA. Hii ni huduma yetu kama KANISA LA SIKU ZA MWISHO, Lazima tuwe na majibu ya KIROHO NA UCHUMI ya dunia yetu kama Yesu na Mitume. Hivyo kuwa na pesa, utajiri na uchumi mzuri NI LAZIMA ili kurahisisha kazi ya INJILI tuliyokabidhiwa katika siku za mwisho. YESU MWENYE ALIKUBALI KUFANYIKA MASIKINI NA AKAISHI MAISHA YA CHINI KWA AJILI YETU, ILI KWA UAMSIKINI WAKE SISI TUPATE KUWA MATAJIRI (2Korintho 8:9). INJILI KUIPELEKA NA KUWAPELEKA WATENDA KAZI VYOTE VINAHITAJI PESA, NI GHARAMA (Warumi 10:13-17).
Asikudanganye wala kukupumbaza mtu, kuwa tajiri na kuwa na uchumi mzuri ni bora mara elfu kuliko kuwa masikini na kuomba omba! Kuwa na vingi kwa utele kiasi cha kugusa na kubariki wengi kwa yale aliyokujalia Mungu ni baraka sana kuliko kuwa katika nafasi ya kupokea misaada. Fedha si mbaya, Bali kuifanya pesa kuwa muungu kwako na ikachukua thamani ya Mungu na muda wa Mungu, hilo ndilo tatizo kubwa! MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, KWA AKILI YAKO YOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA MALI YAKO YOTE. Ukiweza kutimiza hili, PESA HAITAKUPA SHIDA maana utajua kwamba WEWE NI WAKILI TU WA MALI YA BWANA!
Kwa leo niishie hapa, Tafakari na ujifunze, Mwl Dickson Kabigumila. +255 655 466 675 (Kupiga, Whatsapp, text na viber). dicoka@rocketmail.com (email) Website: www.yesunibwana.org

SOMO: UKWELI KUHUSU PESA; SIRI MBILI ZINAZOTAWALA PESA

SOMO: UKWELI KUHUSU PESA; SIRI MBILI ZINAZOTAWALA PESA

UTANGULIZI
Ni jambo la muhimu sana kwa kanisa la siku za mwisho kujifunza kuhusu fedha na uchumi kwa ujumla.

Uamsho unaokuja wa siku za mwisho utakaopelekea KILA GOTI KUPIGWA NA KILA ULIMI KUKIRI YA KUWA YESU NI BWANA utahitaji pesa na vitendea kazi vya mabilioni na matrilioni kuipeleka injili ya Yesu, Kujenga makanisa, kuweka huduma za kijamii; NALIKUWA UCHI UKANIVIKA, NALIKUWA GEREZANI UKAJA KUNIONA, NALIKUWA MGONJWA UKAJA KUNITAZAMA, NALIKUWA NA KIU UKANINYWESHA, NALIKUWA NA NJAA UKANILISHA… Yote haya yatahitaji pesa.
Mwalimu Dickson Kabigumila
Gharama za kuipeleka injili kupitia mitandao, simu, redio, televisheni, satelaiti, website nakadhalika, itahitaji pesa. Lakini pia mahitaji yetu ya kila siku kama Wana wa Mungu yanahitaji na yatahitaji pesa kuyaendesha [Hautanunua sukari, mafuta, ada za watoto, mahitaji ya familia kwa kunena kwa lugha tu]; Fedha itahitajika ili kuleta JAWABU LA MAMBO YOTE.
Hivyo basi na tuanze kwa msaada wa Roho wa Mungu kujifunza siri hizi mbili: 1.Pesa si zile SARAFU AU NOTI… Bali pesa ni THAMANI YA MWENYE NAZO anavyotazama zile sarafu na noti na KUZIPIMA NA KUZIOANISHA na HALI YA UCHUMI ILIYOPO na HALI YA UCHUMI WA UFALME WA MUNGU.

*Rula inapima urefu; Ila rula si urefu, ndio maana hata ukiondoa rula, kama ni sentimeta 2 zitaendelea kuwa sentimeta 2, haziathiriwi na uwepo au kutokuwepo kwa rula.

*Mzani unapima uzito; Ila mzani si uzito, ndio maana kama umepima kitu kina kilogram 5 juu ya mzani hata ukiondoa kwenye mzani pia uzito wake utabaki kuwa kilogram 5.

“Ndivyo ilivyo pesa; kama THAMANI YA MWENYE NOTI AU SARAFU ni kubwa akiwa na NOTI AU SARAFU itabaki kuwa kubwa hata hizo NOTI NA SARAFU zikiondoka. Na ndivyo ilivyo kinyume chake”
NAKUFUNDISHA UCHUMI KWA UFUNUO NA SI VITABU AU KANUNI ZA DUNIA HII. 2. Pesa haikai mahali ambako HAINA CHA KUISHIKA.
Watu wa dunia hii wanaotawala uchumi na pesa wanaelewa wazi kwamba ili pesa ibaki lazima iwe na cha kuishika na kinaitwa “KI/VITEGA UCHUMI” na kadri unavyokuwa navyo vingi ndivyo unavyokuwa na UWANJA MPANA wa kutawala MZUNGUKO WA PESA na KUONGEZA PESA toka mikononi mwa WASIO NA VITEGA UCHUMI… Kwa kifupi, KITEGA UCHUMI ni bidhaa au huduma inayotimiza mahitaji ya watu KWA MABADILISHANO NA PESA toka kwa wahitaji bidhaa au huduma.
HII NDIYO NJIA YA KIBINADAMU ILIYOWEKWA NA MUNGU KUZALISHA FEDHA [Rejea mfano wa talanta]. Kwenye Ufalme wa Mungu:
Mbali ya VITEGA UCHUMI kinachoweza kuishika PESA IKAE ni MUNGU NA KANUNI ZA MZUNGUKO WA PESA alizoweka ambazo zinaitwa UTOAJI.
Mungu kama Mungu binafsi YEYE MWENYEWE ni SUMAKU inayovuta na kunasa uchumi na fedha.

Ukilisoma Neno la Mungu utagundua kwamba, “FEDHA NI MALI YAKE; DHAHABU NI MALI YAKE; VYOTE VIIJAZAVYO NCHI NI MALI YAKE; DUNIA NA WOTE WAKAAO NDANI YAKE”
Hii ni siri ya ajabu kwa mtu anayetaka kuwa na uchumi mkubwa. KITEGA UCHUMI kikubwa na cha kwanza unachokihitaji KUVUTA PESA NA UCHUMI MZURI ni MUNGU ALIYE HAI.
“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya UTAJIRI WAKE katika utukufu katika Kristo Yesu” (Wafilipi 4:19).
“Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, Yaani, Wamchao [BWANA] HAWAHITAJI KITU [kwa maana wana zaidi ya wanavyohitaji toka mikononi kwa BWANA]” (Zaburi 34:9).
“Wana-simba hutindikiwa huona njaa; Bali WAMTAFUTAO BWANA HAWAHITAJI KITU CHOCHOTE KILICHO CHEMA [wana kila kitu na kuzidi]” (Zaburi 34:10).
“…Usije ukamsahau BWANA, Mungu wako AKUPAYE NGUVU [za kiroho, kiakili, kimawazo, kiubunifu, kiuzalishaji, kiafya] ZA KUUPATA UTAJIRI” (Kumbukumbu 8:18).
“UTAJIRI NA HESHIMA ZIKO KWANGU [MIMI MUNGU], Naam UTAJIRI UDUMUO, na haki pia” (Mithali 8:18).
“[Mimi Mungu] natembea katika NJIA YA HAKI, katikati ya MAPITO YA HUKUMU. Niwarithishe MALI wale WANIPENDAO, TENA NIPATE KUZIJAZA HAZINA ZAO” (Mithali 8:20-21). Njia ya pili kwenye Ufalme wa Mungu ya kutunza pesa ni kupitia SADAKA/ UTOAJI:
a)Fungu la kumi (Malaki 3:8-12)
-Kufungua mbingu ziwe wazi upande wa mtoaji
-Kufanya mbingu ziachilie baraka zaidi ya uhitaji na kiwango cha kupokea cha mtoaji
-Kuzuia chanzo cha mapato kisishambuliwe na adui/ alaye
-Kumfanya mtoaji wa fungu la kumi atambulike na kutofautishwa na watu wengine wa kawaida [Na mataifa yote watakuita heri/ aliyebarikiwa]. b)Kutoa kwa masikini/ kumsaidia asiye na uwezo/ aliye na uhitaji (Mithali 19:17, Zaburi 41:1-3, Mithali 21:13).
-Kumsaidia masikini kwa huruma [compassion] ni mkopo kwa Mungu anaolazimika kuulipa; Mungu anachukia madeni, hawezi kukubali kuwa mdeni kwa mtoaji, hivyo lazima alipe na RIBA juu
-Kumsaidia masikini NI UWEKEZAJI KWA AJILI YA SIKU YA TABU [Nyakati mbaya] na itaufanya mkono wa Mungu ukusaidie wakati wa Magumu na taabu.
-Kumsaidia Mhitaji na masikini ni MBEGU itakayotoa matunda WAKATI WA UHITAJI WAKO; Utaita na Mungu atakusikia na kukusaidia
-Kuwasaidia masikini na wahitaji ni njia ya KUWEKA WIGO WA ULINZI wa Mungu kwenye maisha yako, familia, watoto na mali yako.
Ayubu alikuwa BABA KWA YATIMA, MME KWA WAJANE NA JIBU LA WAHITAJI na ikapelekea Mungu KUMJENGEA WIGO dhidi ya kila hila na shambulizi la adui zake. c)Kutoa kwenye Injili, Shughuli za Kuujenga Ufalme wa Mungu / Mambo yanayomhusisha Yesu (Marko 10:28-30).
-Mtoaji ana uhakika wa kupata mara mia hapa duniani [a hundredfold] kwenye kila alichotoa- Inawezekana asipate kwa mkupuo au kwa nmna alivyotegemea kupokea lakini hakika atapata maramia ya kile alichowekeza kwenye injili au Ufalme wa Mungu.
-Ana uhakika wa kupata chochote “alichokisadaka” kwa ajili ya Yesu na injili; Yawe mahusiano [Baba, mama, ndugu wake na waume], Mali [Nyumba, mashamba] nakadhalika mara mia hapahapa duniani.

LAKINI JIANDAE
Utaoji huu una malipo ya juu sana, yanayozidi kawaida hivyo watu wanaokuzunguka hawataelewa “Unafanyafanyaje” kuzungusha uchumi wako, hivyo UTAPATA UDHIA [Kusemwa, kusingiziwa, lawama na kila lisilopendeza] kwa maana kuipeleka injili na Yesu ni KUTANGAZA VITA YA MOJA KWA MOJA NA SHETANI. Ni kuipeleka nuru na kuling’oa giza. Ni kuuondoa Ufalme wa shetani na kuujenga Ufalme wa Yesu Kristo.
KUZIMU YOTE ITAJARIBU KUKUZUIA usiendelee kuleta madhara; UKIONA HIVI KAZA UZI, ONGEZA UTOAJI WAKO… Hii ni sehemu ya utoaji huu wa baraka sana!! Siri hizi mbili zitafakari ni za muhimu sana kwako Mkristo unayetaka kuwa na mahusiano mazuri na Mungu lakini pia kuwa na uchumi mzuri.
Wako Katika Kristo Yesu,
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mawasiliano:
Simu: 0655 466 675 [Kupiga, Whatsapp na meseji] 0753 466 675 [meseji tu] Email: dicoka@rocketmail.com
Website ya mafundisho zaidi: www.yesunibwana.org

KWANINI NI LAZIMA UWE TAJIRI

SOMO: KWANINI NI LAZIMA UWE TAJIRI

KWANINI NI LAZIMA UWE TAJIRI;
1. Yesu ameivunja laana ya torati (kuanzia Kumbukumbu 28:15 na kuendelea, ambayo kati ya laana zilizoko hapo ni umasikini wa kipato na uchumi): Galatia 3:13-14.
2. Yesu amefanyika masikini ili wewe uwe tajiri kwa umasikini wake (2Kor 8:9).
3. Yesu alipofufuka na kushinda mauti, Mfumo wa utawala kwenye ulimwengu wa roho ulibadilika, toka kwa Shetani, na akawa kisheria na mamlaka yote na katika kila eneo (Mathayo 28:18).
4. Kilichomleta Yesu duniani ni “kutafuta na kuokoa kilichopotea” (Luka19:10, Mathayo 18:11), na kati ya vilivyokuwa vimepotea ni Uchumi wa mwanadamu uliokuwa mikononi mwa Shetani (Luka 4:5-7, Mathayo 4:8-9).
Na hiyo kazi pia aliimaliza na kuchukua mamlaka na nguvu ya Shetani kwenye eneo la uchumi (Yohana 17:4).
5. Yesu alipokuwa duniani alitembea kwenye “uchumi mkubwa” na hakuwahi kuwa masikini wa kukosa alichohitaji: Alilisha maelfu kwa chakula kidogo, alitatua matatizo ya kiuchumi kwa hekima ya Kiungu… Na Yesu huyuhuyu anakaa ndani yako na hajabadilika: NI YEYE YULE LEO KAMA ALIVYOKUWA JANA (Waebrania 13:8).
6. Yesu alifundisha kuhusu uchumi kupitia mfano wa “talanta” (Mathayo 25:14-29), na hapo alitufundisha tofauti ya KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA… Wale wawili WALIWEKEZA KILE WALICHOPEWA KAMA MTAJI na wakapata ASILIMIA MIA YA WALICHOWEKEZA (Mwenye tano alipata faida tano, mwenye mbili alipata faida ya mbili), Yule ALIYEIWEKA AKIBA ilibaki hivyohivyo na haikuongezeka. Baada ya muda alikuwa na KIASI KILEKILE ALICHOTUNZA kikiwa kimeshuka thamani kwakuwa fedha hushuka thamani kutegemea muda na dawa pekee ni KUIWEKEZA.
Yesu asingetufundisha siri hii kama anataka tuwe na uchumi mdogo!
7. Yesu hakushughulika na maswala na mahitaji ya kiroho na ya mwili tu ya waliomjia bali pia ALIFANYA MIUJIZA KWENYE ENEO LA UCHUMI PIA… Alifanya muujiza kwenye uchumi wa Petro (Luka 5), Kama uchumi si kipaumbele cha Yesu, asingefanya kitu hiki na miujiza mingi ya kiuchumi.
8. Nguvu ya kupata utajiri na uchumi mkubwa iko mikononi mwa Mungu (Kumbukumbu 8:18).
9. Kama unaamini kwenye BARAKA ZA MUNGU basi amini kwenye UTAJIRI PIA maana “Baraka ya Mungu hutajirisha” (Mithali 10:22).
Huwezi kubarikiwa na Mungu na usiwe na uchumi mkubwa na utajiri wa kutosha.
Ibrahim alipobarikiwa, uchumi wake uligeuka (Mwanzo sura ya 12 na 13:2).
Na Mungu huyu amekupa nafasi ya kuwa “mrithi wa ahadi na baraka za Ibrahimu” (Wagalatia 3:29, Wagalatia 4:28).
10. Mungu tunayemuabudu katika Kristo Yesu ndiye anayehusika na suala la KUTAJIRISHA WATU (Mhubiri 5:19, 1Samweli 2:7-8).
11. Bwana Yesu alisema atatuhukumu siku ya mwisho kwa kutegemea “tuliwavika, tuliwanywesha, tuliwalisha wahitaji na masikini” (Mathayo 25:31-46).
Na haya hayawezi kufanyika ukiwa masikini. Na Mungu hawezi kukupa kazi hii ya kulisha, kuvika, kunywesha, kusaidia wahitaji bila kukupa uchumi mkubwa wa kukurahisishia kazi hii ili akikuhukumu usije kujitetea kwamba ulikuwa masikini.
12. Kama una moyo wa kukubali “majukumu na uwajibikaji” ili kuleta nuru na majibu ya watu wengine, huwezi kuwa masikini (Isaya 60:1-4, 10-11, 16-22).
Ukiwa masikini umetaka, si Biblia wala Ufalme wa Mungu unaotaka uwe masikini.
Amka, lichukue Neno la Mungu na ulidai litimie maishani mwako.
NB: Fuatilia kila andiko na kuliweka katika maombi na matendo, kitaeleweka!
Mwl Dickson Cornel Kabigumila (Mwl D.C.K),
0753 466 675/ 0655 466 675

NADHIRI

MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI NENO; Mhubiri 5:4 “ wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa” Maombi...