NAMNA MADHABAHU ZINAVYOWEZA
KUSHIKILIA MFUMO WAKO WA MAISHA
NENO :Waamuzi 6:24
“Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu
hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya
Waabiezeri.”
Madhabahu ni eneo ambalo linaweza kutumia na
Mungu au shetani ili lijengwe kwa kupitisha nguvu ,mamlaka na utawala wake na
kila madhabahu ina tabia zake.
Madhabahu ni eneo ambalo linakuwa daraja
kutoka ulimwengu war oho kupitisha kilichokusudiwa hadi ulimwengu wa mwili au
nyama.NAmadhabahu zinatenda kazi
kulingana na utawala na mfumo wa mmiliki wao.au kwa lugha nyingine madhabahu ni eneo litumiwalo na watu watu Fulani kwa ajili
ya kufanya ibada zao wakiwa na imani ya nguvu
ya pale,mungu wa eneo lile kulingana na utaratibu wa lile eneo na kila
madhabahu zinategemea na utendaji wa roho wa eneo lile au miungu wa madhabahu
husika.Zipo madhabahu za aina mbili au zenye utawala wa namna mbili,
A)Madhabahu ya MUNGU.
B)Madhabahu ya shetani.
Ili hizi madhabahu zifanye kazi zinategemea
sana
Ø Mungu wa madhabahu
Ø Nguvu ya madhabahu
Ø Sadaka zitolewazo madahahu
husika
Ø Nguvu ya kuhani husika
Sadaka zitolewazo katika madhabahu husika zinauhusianao mkubwa sana na nguvu itokayo
katika madhabau husika juu ya mfumo husika wa maisha yako na maono uliyobeba
juu ya maisha yako ya badae.Na madhabahu ya MUNGU au ya shetani zote zinafanya
kazi kulingana na ene lililopo katika ulimwengu wa roho yani kulingana na
itifaki ya kiutawala juu ya madhabafu husika au mahali pa juu husika katika
ulimwengu war oho.(Yeremia 32.35 “Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo
katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika
moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba
walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda”)
(Waamuzi 6;26 “ukamjengee Bwana, Mungu wako,
madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na
kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata”
Kwa hiyo kila mabdhabahu inataratibu zake na
sadaka zake na ina toa matokeo kulingana na sadaka zitolewazo katika madhabahu
husika.ANGALIZO. “NGUVU YA MADHABAHU HUTEGEMEA SANA KIWANGO CHA SADAKA
ITOLEWAYO KATIKA MADHABAHU HIYO.”Matendo:10;2-4 Kornelio alikuwa
amebeba madhabahu ya Mungu na sadaka zake zilisababisha nguvu za Mungu katika
madhabahu ya Munguiliyokuwa ndani yake
zitoe majibu ya maombi yake ya Muda mrefu mbele za Mungu,,ulishawahi kujiuliza
kama angekata tamaa kutoa sadaka nyingi ingekuwaje? “Akamtazama sana, akaogopa
akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na
kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Sasa
basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro.”hii ina maana kuwa sala zako ziambatanazo
na sadaka katika madhabahu yangu zimefika kikamilifu na sasa majibu ya maombi
yako yanatoaka mahali pangu pa juu..(madhabahu ya Mungu)
Hivyo basi nguvu ya madhabahu kukupa majawabu
ya maombi yako inategemeana sana na sadaka unazotoa katika madhabahu.Madhabahu
ni daraja kati yako inayopitisha vitu kati yako na Mungu unayemtumkia.Swali la
kujiuliza jee unajua upo katika madhabahu gani hata kama umeokoka? yawezekana
hata kama umeokoka bado umevaa Sanda (nguvu ya madhabahu Fulani)Maana
haikutosha tu kufufuliwa kwa Lazaro na Yesu mpaka ilipotolewa amri ya kumvua
sanda..haitoshi ya kuwa wewe tayari unatiketi ya kwenda mbinguni,,,Je mfumo wa
maono uliyobeba yanakwendaje..vipi elimu ipo sawa sawa..maendeleo yako ya
kiuchumi yapo sawasawa..suala la ndoa jee limekaa sawasawa?(Yohana
11.43-44)
Ngoja kushirikishe hili,SADAKA YA MADHABAHU
Kiitifaki sadaka zitolewazo madhabahu Fulani
huwa zinahuisha na kutiisha nguvu ya madhabahu hiyo.Kama upo katika madhabahu
ya Mungu aliye hai unaambatanishwa na vitu vitano ambavyo ndani yake kuna mfumo mzima wa kiiutawala juu ya maisha yako
na maono uliyonayo.Unaambatanishwa na,
Ø Mungu wa madhabahu
Ø Nguvu ya madhabahu
Ø Sadaka za madhabahu
Ø Ibada za eneo hilo
Ø Na kuhani wa madhabahu hiyo.
Ukisoma mwanzo 8;,20-22.” Nuhu
akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika
kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Bwana
akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena
baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni
mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama
nilivyofanya.
Muda
nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari,
wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.”utaona kabisa Sadaka aliyoagizwa Nuhu atoe
zinaachilia mfumo mpya wa maisha yao na ndani yake kuna ibada,sadaka,nguvu ya
madhabahu,kuhani na Mungu mwenyewe.
Madhabahu zote huanzishwa katika ulimwengu
war oho na utendaji wake kuwepo katika ulimwengu wa kawaida au wa nyama.
Madhabahu zinatoa maelekezo ya mfumo wa
maisha yako kwa kujua au kutokujua ndio maana yapo makabila mengi hapa Tanzania
ambayo yana muda maalumu wa kutoa sadaka ila mambo yao yaendea sawia,we unafikiri
ni hali ya kawaida la hasha!Mfumo wako wa maisha umefungwa kwenye
madhabahu.
Madhabahu ya ulimwengu war oho huunganishwa
na madhabahu za ulimwengu wa nyama kupitia
v Sadaka
v Makuhani
v Ibada zifanyikavyo kwa wakati.
MAMBO YAKUUNGANISHAYO NA MADHABAHU HUSIKA.
(1)Jambo la kwanza;SADAKA.
Sadaka
ni njia mojawapo ya kuunganisha maisha yako mwenyewe na wewe mwenyewe na vizazi
vyako katika madhabahu husika ndio maana Yesu alifanyika sadaka ili tuwe na
mamlaka na ukuhani katika Ufalme wa Mungu Ebrania :28” na kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa
sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo
dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu”
Chunguza katiaka ukoo wako kabila ni muda
gani wanatoa sadaka na kwa sababu gani?Uthamani wa sadaka ndio nguvu ya miungu
ya madhabahu husika.Waamuzi 6:25-32 Gideoni alitoa sadaka ili kuwatoa wana wa
Israeli katika miungu Baali na kuwaunganisha na madhabahu ya MUNGU pasipo wao
kujua ndio maana inaleta shida mara baada ya kugundua mungu wa baali hayupo.Na kila sadaka
inautaratibu wake kulingana na nini na kitu gani kinakusudiwa kitokee ndio
maana ukienda kwa waganga wa uchawi wana aina tofauti tofauti ya sadaka
kutokana na matokeo unayoyahitaji,kadhalika
kila madhabahu ina mungu wake na mfumo wake.
Ukisoma Waamuzi 6:29-30 Wakaambiana, Ni nani aliyetenda
jambo hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa
Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili.Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete
mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile
Ashera iliyokuwa karibu nayo Angalia kuitoa madhabahu ya baali
ilisababisha ugomvi juu yao kwa sababu “ameikata”maana yake amewatenga na
miungu baali ya kwao na kuwaunganisha na MUNGU aliye hai.Mifumo ya kiutawala ya
kwao ilitawaliwa na Miungu migeni ndio maana kila mtawala wa wakati ule Israeli
alijiunganisha na miungu baali.
Maisha yako namna yalivyo inawezekana kabisa
ulifungwa kwenye sadaka na kutolewa kwenye madhabahu Fulani,we chunguza habari
ya maisha mlionayo.Unaweza ukaingizwa kwenye mungu wa madhabahu fualani pasipo
wewe kujua badala yake utaona mabadiliko katika mfumo wa maisha
yako.”Kuondolewa kwa madhabahu ya baali iliinua vita vingine si kwa sababu
madhabahu iliondolewa la hasha,bali mfumo wa maisha ya kiutawala juu ya Israeli
umebadilishwa Ezra 3:3 Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa
Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu
kama mtu mmoja.
Ndipo
akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli,
mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa
Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa
juu yake, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, mtu wa Mungu.
Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana
hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea Bwana sadaka za
kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni.Mfumo wa maisha ya Israeli ilisababisha watoe
sadaka itakayowaunganisha na Mungu aliye hai ndio maana wakakusanyika pamoja Je upo
kwenye madhabahu gani inayoamua maisha yako?
(2)Jambo
la pili:Majina uliyopewa yanaweza kabisa kukuunganisha na miungu wa madhabahu
Fulani.wengi wana majina lakini hawajui asili ya majina yao.
Palipo na jina hapo ndipo kuna utambulisho wa
mtu katika vision yake na mfumo mzima wa maisha yako.Adamu alipewa mamlaka ya
kuwapa majina viumbe walioumbwa na Mungu kwa nini,sababu moja wapo utambulisho
wao katoka ulimwengu war oho upo kwenye majina.kadhaliaka future yako
inauhusiano mkubwa sana na jina ulilonanlo sasa.Jamii nyingi hapa wanatabia ya
kurithishana majina wakiamini mhisika
bado yupo na hapo ndipo unapounganishwa
na miungu ya kikabila na kiukoo na mfumo wako wa maisha utakuwa chini ya
madhabahu hizo za kiukoo,na maono yako yamefichwa huko hata kama umeokoka
(mwenye maarifa na afahamu)Mwanzo 2:19-20. Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi
kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone
atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Adamu
akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila
mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
Yakobo nae alibadilishwa utambulisho wake na
kuitwa Israeli maana yake mbarikiwa na Ibrahimu pia kwa nini? Future ya mtu ina
uhusiano mkubwa na jina la mtu,kadhalika na madhabahu zinahusika kabisa na
mfumo wote wa maisha ya mtu hivyo jina ulilonalo yatosha kabisa kuunganishwa na
miungu wa madhabahu husika.Angalia baada ya Abraham kuitwa Ibrahimu Mungu anamwambia maana ya jina lake,,yaani
limebeba nini hapo badae,Mwanzo 17:6-8
Hivyo madhabahu Fulani inatambua vision yako
hapo baadae na kwa kuwa ni chanzo au eneo ambalo linatawala mfumo mzima wa
maisha yako hapo badae basi jina lako linaweza likaunganishwa na madhabahu
fualani.Ndio maana kila jina lina maana si kawaida ila ni utambulisho wa roho
iliyoko kwenye majina Jina lako au maana ya uhai wako upo kwenye nafsi na nafsi
imebeba uhai wako(Roho Mtakatifu akufunulie hili jambo)nafsi ikifa uhai wako
haupo,kadhalika miungu ya giza hushughulika sana na nafsi ya mtu kama ndivyo
utambulisho wako upo ndani ya nafsi na nafsi imeficha jina lako hapo,Basi jina
lako ni njia mojawapo ya kuunganishwa na madhabahu husika.
(3)jambo la tatu.Maagano yaliyowekwa mwanzoni
yatosha kukuunganisha na madhabahu za giza Je kuna maagano mangapi nay a aina
gani ambayo wazazi wako waliweka wakati unazaliwa aidha kupitia kitovu au damu
yako au nywele zako,zilifungwa kwenye miungu gani?si suala la kujiuliza
mpendwa. Yapo maagano ya aina nyingi,lakini agano la damu ni agano lenye
nguvu kwa sababu damu ina sauti,uhai,na damu inatoa laana,Ebra,12:24,Lawi
17;10-12.Kumbuka yapo maagano ya Damu yaambatanayo na sadaka kwa ajili ya ibada
za miungu migeni.
Hivyo damu pia inahusika kabisa katika kuamua
maisha yako ya badae kulingana na maagano yaliyoko katika damu na wewe.Ndio
maana wachawi nao hupenda sana kutumia damu kwa ajili ya kukamata mfumo wa
maisha ya mtu ,nafsi katika madhabahu zao.
Madhabahu nyingi zinakuwa na Nguvu kutokana
na maagano ya damu.Angalia nabii Eliya alivyounganisha kabila 12 za majina
katika Israeli na damu pia.hivyo damu inatosha kabisa kukuunganisha na
madhabahu Fulani.(1Wafamle 18:32-35 Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina
la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu.
Kisha
akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya
kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya
kuteketezwa, na juu ya kuni.
Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni
mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu.
Yale
maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji.)Eliya alifanya hivyo kulingana na uhusika wa madhabahu,na majina Damu na
sadaka Mapipa manne,pande nne za Israeli,wakajaza maji na kumwaga juu
ya juu ya sadaka ya kuteketezwa,mara tatu hesabu yake ni 12 saw na akbila 12 za
Israeli kutoka pande nne za dunia,kiroho maji damu zinashuhudia hapa duniani (1Yoh
5:9) na ndani ya sadaka kuna damu na maji na majina ya isreali KIKABILA
juu ya madhabahu,kwa mantiki hiyo Majina ya Israeli yalifungwa kwenye madhabahu
na sadaka zake na katika sadaka kuna Damu iliyomwagia katika hiyo madhabahu ya
MUNGU.
Watu wengi mfumo wao wa kimaisha unayumba
kutokana na maagano ya damu yaliyowekwa kwenye madhabahu husika ambayo
yamefunga maisha yao katika madhabahu za miungu yao.Wengi huenda hawajua
yakupasa ujue utaratibu wa ukoo wenu na historia ya ukoo wako ili ujue namna ya
kutoka huko.Binafsi ilinigharimu miaka miwili ya maombi kuombea maagano na
familia yangu kiujumla kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu.
Tazama name kipindi cha Nuhu,mara baada ya
gharika jambo la kwanza Nuhu kufanya ni kumjengea Mungu madhabahu ili mfumo
mpya wa kizazi kilichobakia uwe ndani ya madhabahu ya Mungu(Mwanzo 8:20-22. Nuhu akamjengea
Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege
aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Bwana
akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada
ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya
tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama
nilivyofanya.
Muda
nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari,
wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.Mungu atasema Baraka juu ya maisha yao na
majira na nyakati katika mfumo mpya wa
maisha,yote hayo ni baada ya kutoa sadaka ya damu juu ya madhabahu ya Mungu(akatwaa
katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka
za kuteketezwa juu ya madhabahu.) Mungu anasema “Sitailaani nchi tena baada ya
hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu
ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.”maana
yake anaachilia Baraka katika mfumo mpya wa maisha yao.
Madhabahu zimekamata mfumo mzima wa utawala
wa maisha ya mtu.
(4)Jambo
la nne;Viapo vya wakuu wa makabila na miungu yao yatosha kabisa kukuunganisha na madhabahu baali,Hii pia
ni njia mojawapo ya kukuunganisha na miungu ya kigeni ukisoma Habakuki 3:9” Uta
wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti;
Ukaipasua nchi kwa mito”utaona kuwa kuna viapo tosha kabisa juu ya kabila na vina uthabiti
ju ya mfumo wako wa badae.
Angalia Amosi 1;6-8 kufungwa kwa kabila ni
juu ya maaganao au viapo wa miungu yao ya kikabila ndio maana huenda maisha
yako yamefungwa kwenye madhabahu ya kiakabila.
-
Chunguza vizuri katika Amosi 1:6-8 – Hapo unaona kabila zima limepigwa pingu
na kufungwa kisha kutiwa katika mikono ya Edomu (roho ya kuhangaika na kufa
vibaya) nguvu hiyo ya kulifunga kabila zima ilitoka kwenye kati ya miji ile 5
ya wakuu wa Wafilisti (wakuu wa giza) waliokuwa wanatawala miji mitano ya
wafilist. Kwa hiyo kabila zima lilifungwa kwa upako wa giza ulioachiliwa kutoka
kwenye miji 4 ya wakuu wa giza – yaani, Gaza, Ashdodi na Ashkeloni pamoja na
Ekroni.
miungu iliweza kulifunga kabila zima. Je! Iliwezekanaje kukamata kabila
lote na kulifunga? Kwa kupitia mtu mmoja (mkuu wa kabila) miungu ikalifunga
kabila.
Wakuu wa giza hushughulika sana na wakuu wa
makabila na Mungu nae hushughulika pia na wakuu wa kabila waliobeba kabila
Fulani.Angalia vipaumbele vya kabila 12
za Israeli.
Mwanzo 49;3-4 Reubeni, u mzaliwa wangu wa
kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na
kwa nguvu.
Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu,
Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia
kitanda change Reuben alipozini na mke wa
babaye iliharibu hatima ya kizazi chake ,nachotaka ujue Mungu huangalia
waanzilishi wa kabila na si watakaofuata…mfumo wa badae wa kizazi cha Reuben
uliharibika kutokana na Reuben mkuu wa kabila la Reuben.
Leo hii hayo mambo yapo hiyo ni madhabahu ya
uasherati iliyowekwa na waanzilishi wa kabila lako,huenda kuna mambo ambayo
hujapata ufumbuzi mpaka sasa fuatilia habari ya kabila lako na viapo
vyao.Reubeni alikuwa ndiye mzaliwa wa kwanza lakini Baraka zote alipewa Yusuph
nduguye,vipo viapo vingi vya kabila lako ambavyo vilikuunganisha na madhabahu
ya baali na mpaka sasa inashughulika na maisha ya vizazi vyako mpka Mungu
mwenyewe aingiie kati.(1Nyakati 5:1-3. Na wana wa Reubeni, mzaliwa
wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa
kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa
wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo
haki ya mzaliwa wa kwanza.)
Kwani
Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala;
bali haki ile ya mzaliwa wa kwanza
alipewa Yusufu);
(5)Jambo
la tano.Kuingia katika eneo ambalo wanaabudu miungu mingine yatosha
kukuunganisha na madhabahu zao
.Waamuzi 2;11-13 Wana wa Israeli walifanya
yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba
zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi
ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele
yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.
Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.Kama umeokoka na hauna stamina ya kiimani
katika Kristo ndani yako na nguvu ya Roho Mtakatifu ni rahisi sana kuruhusu
madhabahu nyingine iingilie na kutawala mfumo wa maisha yako ya kiroho.Inategemea
sana na nguvu ya Mungu itendayo kazi ndani yako binafsi au upako wa Mungu juu
yako binafsi.
Wana wa Israel waliingia kwenye miungu ya
kigeni kutokana na upako wa viongozi wao ndio maana walipoachwa walianza
kuabudu miungu migeni ya madhabahu za kigeni.fuatilia tangu walipoanza
safari toka Misri,kukaa kwao kiimani
kulitegemea sana na imani na uimara wa kiongozi waona si wao wenyewe haijalishi
waiweka maagano ya namna gani na Mungu na kwa kiwango gani.,
(6)jambo
la sita.Kujiingiza kwenye agano la ndoa unaachilia mfumo mpya wa utendaji kazi
ndani yako.Unapoingia kwenye suala zima la ndoa yapo mambo ya msingi sana
ya rohono yakupasa ushughulikie kabla ya
ndoa ili imani yako katika Kristo Yesu iwe thabiti.maana unapoingia kwenye ndoa
ni agano lingine la kiamisha kwako na lina uhusiano mkubwa sana na maisha yako
ya kiroho.Waamuzi 3;4-7 Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua
kwamba watasikiliza amri za Bwana, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa.
Basi
wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao
Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi;
wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe
wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao.
Wana
wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakamsahau
Bwana, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtoreth .Kujiingiza kwa Waisraeli katika ndoa
ilikuwa njia tosha ya kuwafunganisha na madhabahu za miungu mingine,kitendo tu
cha kuoa au kuolewa yatosha kukuingiza kwenye madhabahu nyingine isipokuwa
umepata ufahamu juu ya jambo hilo.
Ndoa ni eneo tosha la kubadili mfumo wako wa
maisha kuwa mazuri au mabaya,Israeli waliruhusu mungu baali na maashtoreth
kupitia ndoa na kila madhabahu ina Mungu wake na tabia zake.
Suleiman alipooa wanawake wa kigeni
walibadili imani yake mbele ya madhabahu ya Mungu(1Wafalme 11.1-8 1 Mfalme Sulemani
akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa
Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,
na wa
mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie
kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani
akaambatana nao kwa kuwapenda.
Akawa
na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza
moyo.
Maana
ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu
mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa
Daudi baba yake.
Kwa
kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo
la Waamoni.
Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa
Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la
Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo
la wana wa Amoni.
Na
kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza
uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.)”You must not intermarry with them because
they will surely turn your heart after their gods..hii ni sababu tosha ya
kulinda imani yako kwa Kristo ili usije ukaingia katika madhabahu za baali.na
kujifunganisha kwa kutoa sadaka.
Tambua kuwa unapoanza agano la ndoa kuna kuwa
na mifumo tofauti ya kiutwala katika maisha yako
Baadhi ya miungu na harakati zake juu ya
makabila ya Israel 2Falme 23:13.( Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi,
wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa
mbili za nyumba ya Bwana, mfalme akazivunja, akazitelemsha huko nje, na
kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya
Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga
Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi,
chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.
Akazivunja-vunja nguzo, akayakata-kata
maashera, akapajaza mahali pake mifupa ya watu)
1. Ashtoreshi – alikuwa mungu mke wa kabila la wasidoni,
kama inavyoonekana katika 1 Wafalme 11:33. Ashtoreshi ni kirefu cha “Ashera”
ambaye pia aliaminiwa kuwa ni mungu anayefanikisha uzazi wa kila kitu. kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu
Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu,
mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni
pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake.
2
Kemoshi –
alikuwa mungu wa wamoabi – mungu kemoshi na baal – peori ni miungu iliyowatesa
sana kabila la moabi hata kwa kuwafanya kuwa waasherati na wazinzi – Hesabu
25:1 – 3. Basi Israeli akakaa Shitimu,
kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;
kwa
kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao;
watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.
Ikawa
Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.
Kisha
Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu
hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli.
Basi
Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake
waliojiungamanisha na Baal-peori.
Na
tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze
mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa
wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania.
3.
Milkomu au moleki – alikuwa mungu wa Amoni. Moleki alilitawala na kulikandamiza kabila la
waamoni. Mungu moleki ndiye aliyelifanya kabila la waamoni kuamini kwamba,
wakitoa sadaka ya kafara ya watoto watafanikiwa na kuwa karibu na mungu – Lawi
20:1 – 5( Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
Tena
uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au
miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na
kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.
Mimi
nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake; kwa
kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu
pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.
Tena
kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yo yote, hapo atoapo
katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue;
ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na
jamaa zake, nami nitamkatilia mbali, na hao wote wamwandamao katika uzinifu,
ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao) 2Falme 17:17 ndiye anayeongoza ibada za
sadaka za watoto mpaka leo, na sadaka za mimba changa. Sulemani alipomuoa mke
wa Amoni bila kujua miungu ya chimbuko lake, ghafla nafsi yake ilinaswa katika
ulimwengu wa giza na akaanza kujenga madhabahu kwa ajili ya mungu Moleki. Na
kuanzia hapo miungu 4 ilianza kummiliki – 1Falme 11:5 -7.
Unaposoma 1Falme 11:3-8” Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao
wakeze wakamgeuza moyo.
Maana
ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu
mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa
Daudi baba yake.
Kwa
kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo
la Waamoni.
Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa
Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la
Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo
la wana wa Amoni.
Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake
wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.”
-
Unagundua kuwa, nafsi ya Mfalme Sulemani ilifungwa pingu na miungu 4.
Ø Ashtoreshi – mungu mke wa wasidoni
Ø Milkomu au moleki – mungu wa Waamoni
Ø Kemoshi – mungu wa Wamoabu
Ø Baal – miungu ya Wafilisti ambayo aliitolea sadaka.
(7)Jambo la saba.Maagano ya kinadhiri
yaliyoweka wakati ukiwa tumboni mwa mama yako au kabla hata ya wewe katika
ulimwengu huu wa mwili.Hili ni jambo linine ambalo linatosha kabisa
kukufunganisha kabisa na madhabahu Fulani.Wapo wazazi kabla ya wewe kuzaliwa wa
huenda wanaipitia eneo gumu la kukupata wewe,wanafikia sehemu ili uzaliwe
wanaweka agano la kinadhiri kwa miungu Baali au Mungu aliyehai hivyo kiroho kwa
namna moja au nyingine unakuwa umeunganishwa na madhabahu husika kabla yaw ewe
kuzaliwa.Nimeona watu wanapata matatizo ambayo yanatokana na madhara ya wao
kuunganishwa kwenye madhabahu za miungu baali na maisha yao yanakosa muelekeo
kwa sababu uhai wa maisha yao ya badae umefungwa katika madbahahu ya miungu
baali.Kadhalika kwa Mungu pia ni hivyo hivyo,Tazama habari za Hana kabla ya
Samweli kuzaliwa alikwisha muunganisha na madhabahu ya Mungu(1Samweli 1:11 Then she made a vow and said,O Lord of
hosts if you will indeed look on tha afflication of your maidservant and
remember me and not forget your maidservant,but will give your maid servant a
MALE CHILD then I will give him to the Lord all days of his life and no razor
shall come upon his head”)hiyo lilikuwa agano la kinadhiri ambalo
ilimsababisha Mungu kumjibu Hana na kuzaliwa kwa mtoto mume Samweli na badae
anampeleka madhabahuni kwa kuhani Eli angalia na jina alilompa mwanae,lilikuwa
na muunganiko kiroho na agano ambalo aliweka kwenye madhabahu ya Mungu na Mungu
anapata nafasi ya kupitisha nguvu zake hapo kwa ajili ya taifa la Israeli(1samweli
1:22) kwa hiyo ni vema sana ukajua namna ya mfumo mzima wa wewe
kuzaliwa na kaa na wazazi wako uwaulize habar zako kabla yaw ewe kuzaliwa,wapo
wanaotaka wazaliwa wao wa kwanza wamtumikie Mungu na ndio maana unajikuta upo
nyumbani mwa Mungu na vita vyake vya rohoni si vya kawaida.
NAMNA GANI UTAJINASUA NA MIUNGU BAALI?
Mruhusu Mungu Akupe maeneo ya kushughulikia
kimaombi maana usiende kwa namna unavyofikiri kushulika na madhabahu nyingine
maana inahitaji sana nguvu za MUNGU
Hili jambo si la kawaida na si krahisi kwa
sababu ya vitu vilivyowekwa na kukuunganisha na madhabahu za miungu
baali.Tazama nami Waamuzi 6;25 Maelekezo anayoyapokea Gideon juu ya kuvunja
madhabahu za baali amtwae ng’ombe maana yake kuwa sadaka ya Damu kwa agano la
kale lakini sasa ipo Damu ya Yesu pekee ya kukutoa katika maagano hayo ya
miungu baali yanayoshikilia mfumo mzima wa maisha yako’sasa kila madhabahu
inatabia na mifumo yao na Mungu pekee ndie atakayetoa ufahamu na maarifa ya
kutoka huko kwenye madhabahu za baali.
Madhabahu zinaweza wakilishwa na vitu
mbalimbali mfano miti mikubwa(mwanzo 21;33),kwenye milima(kutoka 3:12 Yohana
4:20)ndio maana yakupasa uombe muongoze kwa Mungu mwenyewe namna ya kutoka
huko.
Upo
uhusiano mkubwa sana kati ya maisha yako binafsi na madhabahu husika na kila
moja inafumo wake. Angalia madhabahu aliyoibeba Yesu kipindi anazaliwa Je
ulishawai kujiuliza kwa nini Herode aliagiza watoto wa miaka miwili tena
wakiume wauawe?Ukienda pasipo utaratibu wa Mungu juu ya madhabahu
ulioko,kujinasua italetashida isipokuwa kwa njia y Yesu tu
Ndani ya Yesu kulikuwa na mfumo wa kitwala
kifalme rohoni na ulimwengu wa nyama
Mifumo miwili ya kiutawala yenye kutofautiana
kiitifaki haiwezi kukaa pamoja hata siku moja.
MUNGU AKUBARIKI SANA NA AKUPE UFAHAMU NA
UELEWA ZAIDI JUU YA MASUALA MAZIMA YA MADHABAHU
Mwl.Fredrick J Lupenza.