Mithali 24:10
“UKIZIMIA SIKU YA TAABU, NGUVU ZAKO
NI CHACHE”
- Msingi wa Kwanza
Tambua utendaji wa malaika wa Bwana katika
eneo la kukutia nguvu ya Kumaliza kazi uliyoianzisha au jambo
Tazama hapa Luka 22:42-43 “Ee Baba ikiwa ni mapenzi yako uniondolee
kikombe (kazi aliyokuwa amekwisha ianza Yesu ya kuelekea msalabani) hiki
walakini si mapenzi yangu bali mapenzi yako yatendeke 43.Malaika mbinguni
akamtokea, AKAMTIA NGUVU”
Na katika hilo jambo lako “Jiulize kama ni mapenzi ya Baba aliye
mbinguni au la kwako”! kwa sababu hiyo utagundua kuwa “kuna mvutano wa ndani
kati ya Roho yako na Mwili wako kati kati ya nafsi yako inayo katibu habari
kati ya mwili na roho yako” Kwa kuwa roho I radhi lakini mwili ni dhaifu
Kutoka 23:20,23,
“Tazama , mimi namtuma malaika aende mbele
yako, ili akulinde njiani(Akutie nguvu ya kumaliza jambo si tu kukulinda) na
kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengenezea 23.Kwa kuwa malaika wangu
atatangulia mbele yako na kukufikisha kwenye Mwamori, na mhiti, na Mperizi, na
Mhivi, na Myebusi nami nitawakatilia mbali”(Soma pia na Kutoka 23:27-30,
Ebrania 1:14, Zab 91:11, 34:7-8)
Tazama pia habari za Petro gerezani “alikaa gerezani akiwa amefungwa
minyororo pamoja na walizi wa kumlinda walikuwepo lakini kwa maombi ya kanisa
bila kukoma ikamsukuma Mungu kutuma Malaika wake Kumtetea kwa sababu kazi
ilikuwa bado hajaimaliza” (Mdo 12:5-10), kwa mantiki hiyo Jifunze pia kusukuma
jambo lako kwa namna ya Maombi ambayo yanaachilia utendaji wa Mungu kwenye hilo
jambo na kulikamilisha hakika (ukimwita Mungu kila wakati, palipo na ugumu
huingilia kati na kufanya wepesi katika hilo jambo ambalo umelianzisha)
Mungu Akubariki sana..Itaendelea Msingi wa Pili..