Sunday, 27 July 2014

MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI





MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI
NENO;
Mhubiri 5:4 “wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa”
Maombi ya nadhiri ni maombi afanyayo mtu kwa hiari ya moyo wake juu ya jambo Fulani na unaachilia ahadi ndani ya moyo wako ambayo itamsukuma Mungu kujibu maombi yako sawasawa na muda ambao Mungu anatimiza ahadi yako.au
Ni maombi afanyayo mtu kwa hiari yake mwenyewe na Mungu anayemtumkia  kiasi cha majibu yake yamefichwa katika ahadi  ya hiari kati yake na MUNGU ambayo ndio patano lake na MUNGU. Akitafuta sana mwongozo wa Mungu, Yeftha anaweka nadhiri hii kwa Mungu: “Hakika ukiwatia wana wa Amoni mkononi mwangu, itatukia pia kwamba yule atakayetoka nje, atakayetoka nje ya milango ya nyumba yangu kuja kunipokea nitakaporudi kwa amani kutoka kwa wana wa Amoni, lazima atakuwa wa MUNGU, nami nitamtoa huyo kuwa toleo la kuteketezwa.” Waamuzi 11:30-33.
Roho ya Mungu ilikuwa ikitenda juu ya Yeftha alipoweka nadhiri hiyo, na pia MUNGU alibariki jitihada zake. Maandiko yanamsifu Yeftha kwa sababu ya imani yake na kwa yale aliyofanya kuhusiana na kusudi la Mungu. (1 Samweli 12:11; Waebrania 11:32-34)Kwa hiyo, hangefikiria hata kidogo kumtoa mwanadamu awe dhabihu. Kufanya hivyo ni uuaji. Hivyo basi, Yeftha alikuwa akifikiria nini alipoweka nadhiri ya kumtoa mtu kwa MUNGU?NADHIRI ZAKO MBELE ZA MUNGU ZISIZIDI UWEZO WAKO KIIMANI ILI KUTIMIZA
Ni wazi kwamba Yeftha alimaanisha kuwa angemtoa yule ambaye angekuja kumpokea ili amtumikie Mungu kikamili.
Hiyo ni nadhiri ambayo Yeftha aliweka kwa MUNGU..na Mungu akafanikisha..Angalia habari za Yakobo  kaweka nadhiri na ikamsukuma Mungu kujibu (Mwanzo 28;20-22)
USIWEKE NADHIRI MBELE ZA MUNGU KAMA ROHO WA MUNGU HAJAKUSHUHUDIA NDANI YAKO MATOKEO YAKE UTAKUWA NA DENI MBELE ZA MADHABAHU YA MUNGU.
VIPENGELE VYA NADHIRI MBELE ZA MUNGU
A)uwe na hoja yenye nguvu mbele za MUngu  au neon lenye nguvu isaya 41:21
B)uwe na sadaka ya hiari maana sadaka yako ni patano timilifu mbele za MUNGU.Mwanzo 28;20,1Samw.1;10-12
c)uwe na muda  muafaka wa kutoa nadhiri yako iliyobeba maombi yako
d)ukiweka nadhiri yako hakikisha unaitoa na usiweke nadhiri kama ndani yako huna uhakika wa kuitimiza maana ni suala lenye gharama kwako.Kumb.23;21-23,Zab 50.14
e)Usitoe nadhri yako mahali ambapo Mungu hajapatana nawe…kama umwemwaidi Mungu kumtolea eneo Fulani usitoe kinyume na patano lako na Mungu kwa itabaki kuwa deni mbele ya madhabahu ya MUNGU.Mwanzo 31:13,17,hesabu 30;3-16.
kumbuka yapo madhara ya kutotimiza nadhiri yako kwa MUNGU moja wapo ni
Anania na safira waliweka nadhiri yao ya kuuza kiwanja na kukabidhi fedha ila baadaye waliona tamaa na kutoweza kutimiza nadhiri yao, matokeo yake ni kifo.Unaishi katika mashaka na wasiwasi muda wote kwani nadhiri yako hujaitoa kwa Mungu.Matendo ya mitume 5:1-11..Maendeleo ya kiimani na kiuchumi yanadumaa kutokana na kutotimiza nadhiri yako.

Mungu akubariki sana
 Na mwl.Fredrick J Lupenza

NADHIRI

MAOMBI YA NADHIRI YAAMBATANAYO NA SADAKA YA NADHIRI NENO; Mhubiri 5:4 “ wewe ukimwekea Mungu nadhiri ,usikawie kuiondoa” Maombi...